Na Mwandishi wetu- Ngorongoro

Wazee wa kimila jamii ya Maasai na viongozi wa dini katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, wamelaani kitendo cha waandishi wa habari na watumishi wengine wa serikali kushambuliwa.

Tukio hilo lilitokea Agosti 15 mwaka huu katika kijiji cha Enduleni wakati watumishi wa serikali na waandishi wa habari wakiwa katika majukumu yao.

Viongozi hao kwa pamoja wakiwa wamekutana katika kijiji cha Kapenjiro, wamesema wamemuomba Mungu aweze kuwasamehe watuo hao waliofanya kitendo  hicho kwa kuwa hawajui watendalo.

Katekista Edward Leiyan kutoka Parokia ya Nainokanoka,  amesema kwa niaba ya wakazi wa Ngorongoro wanawaombea Msamaha  waliofanya kosa hilo kwa kuwa Mungu hapendi Mikono inayomwaga damu, macho yenye kiburi, Ulimi wa Udanganyifu na Miguu inayokimbilia katika uovu.

Naye kiongozi wa mila Keswai Mepukori, amelaani vikali kitendo hicho na akisema hataki kitokee tena baada ya upatanisho walioufanya.

Viongozi hao wa kimila na Kiroho, wamechinja Ngombe watatu, mmoja kumwaga damu ishara ya kuomba radhi kwa uongozi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro 

Ng'ombe wa pili kwa ajili ya kuomba radhi kwa Serikali na waandishi wa habari kwa tukio lililotokea la kuwashambulia Waandishi wa habari ambao hawana hatia.

Ng'ombe wa tatu ni kwa ajili ya kumuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa tukio hilo huku akiwa na nia njema ya kuwafanya wananchi hao wawe na maisha mazuri katika maeneo salama yenye huduma stahiki.


Share To:

Post A Comment: