Katika kipindi cha Mwaka 2022/2023, Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) ilifanya ukaguzi Ukaguzi kwenye Vyama vya Ushirika na jumla ya Vyama vya Ushirika 4,712 vilibainika kuwa na mapungufu mbalimbali ya kiutendaji, na baada ya mapungufu hayo yalifanyiwa kazi kwa kuchukua hatua mbalimbali za kinidhamu.

Kauli hiyo imetolewa na Mrajisi wa Vyama vua Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)DKT. Benson Ndiege wakati akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dodoma kuhusu Utekelezaji na Vipaumbele vya Tume hiyo kwa mwaka wa Fedha 2023/2024.

Aidha Dkt.Ndiege amebainisha hatua zilizochukuliwa ni kuvunja bodi 55 za Vyama vya Ushirika, kupeleka masuala 30 polisi na masuala 47 yanashughulikiwa na TAKUKURU pamoja na kutoa mafunzo kwa watendaji 4,732 wa Vyama vya Ushirika.

Dkt Ndiege mesema kuwa Hadi kufikia Juni 30, 2023, jumla ya kilo 1,826,850,970 sawa na tani 1,826,850.97 zenye thamani ya Shilingi Trilioni 1.75 ziliuzwa kutoka kwenye mazao ya tumbaku, korosho, pamba, kahawa, ufuta, kakao, mkonge, chai, mbaazi, soya, zabibu, miwa na maharage

''jumla ya kilo 1,826,850,970 sawa na tani 1,826,850.97 zenye thamani ya Shilingi Trilioni 1.75 ziliuzwa kutoka kwenye mazao ya tumbaku, korosho, pamba, kahawa, ufuta, kakao, mkonge, chai, mbaazi, soya, zabibu, miwa na maharage.''amesema Dkt Ndiege

Hata hivyo katika kutekeleza majukumu kwa mwaka wa fedha 2023/2024 tume hiyo inafanya mchakato wa uanzishwaji wa Benki ya Taifa ya Ushirika ili kuviwezesha Vyama vya Ushirika kupata Mikopo yenye Riba nafuu na kufikia Disemba 2024, Tume itakuwa imeshazindua Benki ya Taifa ya Ushirika (KCBL) na kuwa mali ya wanachama katika kujipatia mikopo ya kuendesha shughuli zao kikamilifu.

Share To:

Post A Comment: