Na; Elizaberth Paulo, Dodoma


Tanzania imebahatika kuwa mwenyeji wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika( African Food System Forum) kwa mwaka 2023.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. David Silinde amesema hayo leo Agost 5, 2023 Jijini Dodoma alipokua akifungua Maonesho na Mashindano maalum ya Mifugo Kitaifa katika viwanja vya Nzuguni akitumia hadhara hiyo kutangaza fursa hiyo iliyoipata nchi.

 

Mhe. Silinde amesema Mkutano wa Jukwaa hilo unatarajiwa kufanyika tarehe 5-8 Septemba, 2023 Jijini Dear es salaam huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa Jukwaa na kwamba ni fursa kubwa ya kuvutia uwekezaji katika sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kuitangazia Dunia uwezo wa nchi kuzalisha na kulisha Afrika na Dunia kwa ujumla.


“Rai yangu kwa wadau wote wa sekta hizi hususan sekta binafsi ni kuwaomba mshiriki katika jukwaa hilo linalotarajiwa kuwa na washiriki wasiopungua 3,000 kutoka nchi mbalimbali.”Amefafanua Naibu Waziri Silinde

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: