Na; Elizabeth Paulo, Dodoma 

MKUU wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, amesema kuwa mkoa huo unategemea zaidi pato litokanalo na kilimo, mifugo  na Uvuvi na kueleza kuwa kutokana na hali hiyo maonesho ya nanenane yatakuwa chachu katika kusukuma maendeleo kwa kutumia teknolojia zitakazooneshwa.



Amesema kuwa mkoa wake kwa sasa unaendelea vizuri katika suala la kuwa na kilimo bora na  cha kisasa na kusababisha kuwa na ziada ya chakula cha kutosha.


Serukamba ametoa kauli hiyo  wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya wakaulima, wafugaji na Wavuvi yaliyofanyika kikanda katka viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma .



Amesema kuwa shughuli za kilimo zinaendelea kutekelezwa ikiwa ni pamoja na kujihakikishia usalama wa chakula na malighafi ya kulisha viwanda vilivyopo.


Aidha amesema kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani 477,967 mwaka 2016/17 hadi kufikia tani 726/771.3 mwaka 2021/2022 na kuwa na ziada ya tani 184,595.6 kutokana na makadirio ya idadi ya watu 2,008,058 waliopo katika mkoa.


Mbali na hilo amesema kuwa uzalishaji wa mazao ya biashara umeongezeka kutoka tani 151,965 mwaka 2016/17 hadi kufikia tani 342,405.5 mwaka 2021/22.


Amesema  katika mwaka wa fedha wa 2023/24 serikali imeupatia mkoa wa singida kiasi cha sh.bilioni 34.17 kwa ajili ya ujenzi wa Sikimu ya umwagiliaji ya msingi iliyopo wilaya ya Mkalama yenye jumla ya Ekari 2,000 na sh.bilioni 1.8 kwa ajili ya kuanza shughuli za awali za ujenzi wa skimu ya Tyame,Masagi iliyopo wilaya ya Iramba yenye jumla ya Ekari 4000.


Miradi mingine itakayo anza kutekelezwa katika mwaka 2023/24 katika mkoa wa Singida ni pamoja skimu 15 zenye jumla ya ekari 13,833 zitafanyiwa upembuzi yakinifu ,usanifu na ujenzi ,skimu 12 zenye jumla ya ekari 7285 zitakazofanyiwa upembuzi na ukarabati , mabwawa 6 yatafanyiwa upembuzi yakinifu usanifu na ujenzi ambayo yatamwagilia eneo lenye jumla ekta 4900.


“Tunaratajia kuwa baada ya kukamilika baada ya utekelezaji wa miradi mkoa utakuwa na eneo lenye jumla ya ekta 32,018 za umwagiliaji sawa na asilimia 65.85 zenye eneo lote la ekta 47,000 zinazofaa kwa umagiliaji zilizopo na wakulima 80,045 watakao nufaika.


“Mkoa wa Singida kwa kushirikiana na wadau wa kilimo na ufugaji, utaendelea kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji juu ya matumizi ya kanuni bora za kilimo na ufugaji .


“Matumizi ya pembejeo za kilimo na ufugaji yanasisitizwa ili kuhakikisha kuwa tija ya uzalishaji inaongezeka , katika kipindi cha mwaka 2022 /23 kiasi cha tani 395 .38 za mbegu za alizeti ruzuku ya serikali y ash.bilion 3.1 zilizopelekwa na kutumika na wakulima.


“Aidha mbolea yenye ruzuku ya serikali kiasi cha tani 2973 zenye thamani y ash.bilioni 4.1 zilizopokelewa na kutumika na wakulima, katika sekta ya mifugo jumla ya lita 2664 za madawa ya kuogesha mifugo zenye thamani ya shilingi 119,880,000 zilizopokelewa na kutumika na wafugaji”ameeleza Selukamba.


Akiendelea kutoa taarifa ya Mkoa wa Singida Serukamba alisema kuwa jumla ya Majosho 34 yamejengwa kwa gharama y ash.742,000,000 na kueleza kuwa Mkoa utaendelea ushirikiana na wadau ili kuhakikisha pembejeo za kutosha zinapatkana na kuwafikiwa wanufaika wanufaika kwa muda muafaka ili kuhakikisha kuwa tija ya uzalishaji inaongezeka katika sekta za milimo na mifugo.


Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rossemery Senyamule wakati wa kufungua maonesho hayo amesema kuwa maonesho ya yalenge kuwa patia elimu wakulima, wafugaji na wavuvi kwa lengo la kuwanufaisha katika kuendesha ufugaji na kilimo chenye tija zaidi.


Hata hivyo Senyamule amesema kuwa maonesho ya Nanenane kanda ya kati yamekuwa na ubunifu mkubwa kwa maana ya kuwa na makongamano ya kutoa elimu juu ya kilimo cha Alizeti,Mtama na Kuku kwa lengo la kuwapatia elimu wakulima ili kuweza kuwa na kilimo chenye tija badala ya kuendesha kilimo cha kujikimu.


Aidha amewataka wadau wote wa kilimo kuhakikisha wanashiriki kwa uaminifu kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ambayo yatwafanya kujiongezea kipato wao, jamii na taifa kwa ujumla wakati wa utekelezaji wa shughuli zao za masuala yanayihusu kilimo, ufufani na uvuvi.

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: