Na John Walter-Babati.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga ameweka jiwe la Msingi ujenzi wa madarasa matatu na ofisi moja katika shule ya Msingi Gidewari Wilayani Babati.

Ujenzi huo unafanyika kwa fedha kutoka Mamlaka ya elimu Tanzania (TEA) Shilingi Milioni 71,372,640 na nguvu za wananchi wa Kijiji Cha Gidewari Kata ya Dabil shilingi Milioni  8,100,00.

“Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan  imelenga kuboresha huduma za elimu  na Afya tumuunge mkono” alisema Sendiga 

Sendiga amesema serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya Elimu katika shule za Msingi na Sekondari.

Share To:

Post A Comment: