MKUU wa Mkoa kilimanjaro Nurdin Babu ametoa wiki mbili kwa kamati ya ujenzi kuhakikisha wanasimamia hatua za  mwisho (finishing) kukamilika kwa haraka jengo la wagonjwa wa nje (OPD) Maabara na nyumba ya mtumishi katika zahanat ya Naibili


Ameyasema hayo akiwa kwenye ziara  wilayani  Siha mkoani Kilimanjaro akikagua  miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya sita chini Rais Dk.Samiha Suluhu Hassani

Amefafanua Rais Samia ametoa fedha Sh. 271,096,536.00 lengo wananchi wake wapate huduma za afya kwa wakati."Sipo tayari kuona ujenzi huo, kamati ya usimamizi unasuasu,  hivyo naagiza kituo hicho kijegwe usiku na mchana, "amesema Babu.

Mbali na hayo yote Mkuu wa Mkoa amewataka kila kiongozi kwa nafasi yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha kujua kila mradi unaotekelezwa katika sekta yake na kusimamia kwa ukaribu na kuhakikisha mradi unamalizika ukiwa na viwango vya hali ya juu.


Share To:

Post A Comment: