Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mashindano maalum ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA yameanza rasmi leo Jumapili Agosti 27,2023 ambapo timu ya Ngokolo Sekondari imeibuka na ushindi wa magoli matatu dhidi ya timu ya Chuo cha St. Joseph ambayo haikupata goli katika uwanja wa SHYCOM.

Mashindano hayo yameandaliwa na taasisi ya Bega kwa Bega kwa kushirikiana na jumuiya ya vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini.

Akizungumza mratibu wa mashindano ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA,  Jackline Isaro amewapongeza wadau mbalimbali na wananchi waliojitokeza kwenye mechi hiyo ambapo ametaja timu zitakazocheza kwenye mchezo unaofuta.

“Niwaombe wananchi wapenda burudani waendelee kujitokeza na kila siku tutakuwa tunakabidhi jezi kwa timu ambazo zinafuata leo tumekabidhi jezi peya saba ili waweze kwenda kujiandaa vizuri”.

“Mechi ya pili itakayofuata ni timu ya Mnara wa Voda dhidi ya timu ya Wapiga debe mchezo huo utachezwa katika uwanja wa SHYCOM, mechi ya tatu ni Ngokolo FC dhidi ya Kadunda, mchezo namba nne utakuwa ni timu ya Mwawaza na timu ya Ndala lakini mchezo mwingi ni timu ya mjini Shinyanga na timu ya Bushushu kwahiyo tutaendelea kutoa ratibu”.amesema Mratibu Jackline Isaro

Mgeni rasmi katika mechi hiyo ni mjumbe wa kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Benard Reuben Shigela ambaye amezipongeza timu hizo kwa kumaliza mchezo salama.

Kwa upande wake katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Shinyanga ambaye pia ni mratibu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Mkoa wa Shinyanga Bwana Seleman Magubika naye amewapongeza waandaji wa mashindano hayo, Jumuiya ya vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini kwa kushirikiana na Taasisi ya Bega kwa Bega ambapo amewaomba kuendelea kuwekeza katika michezo.

 

Awali wakati wa timu ya Ngokolo sekondari ikicheza na timu ya chuo cha ST. Joseph leo Jumapili Agosti 27,2023 katika uwanja wa SHYCOM mjini Shinyanga.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: