Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ametoa rai kwa wananchi hususani wakazi wa Kata za Mbezi, Ubungo na Msakuzi Kusini na Kaskazini ya jijini Dar es salaam ambao ni wanufaika wa mradi wa maji wa Mshikamano kuwa na subira ya kuunganishiwa huduma ya majisafi katika makazi yao kwa kuwa kazi ya ufundi huwa inatekelezwa kwa kuzingatia taratibu na weledi.

Amesema hayo alipokagua utekelezaji wa mradi wa maji wa Mshikamano uliotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).Amesema kuwa mradi wa Mshikamano umetekelezwa kwa ufanisi mkubwa na DAWASA na lengo ni kujibu shida ya majisafi kwa wananchi.

"Tumesikia shuhuda nyingi kutoka kwa wananchi kuwa maeneo haya yalikuwa na upungufu wa maji kwa mrefu, lakini kwa jitihada kubwa za DAWASA maeneo mengi yameanza kupata maji, tunaishukuru DAWASA kwa namna ambavyo wanaiwakilisha vizuri Wizara ya Maji."Mhandisi Maryprisca amesema.

"Wito wangu kwa wananchi ambao wameshalipia maunganisho ya maji wawe na subira kwa kuwa kazi za kiufundi zinatekelezwa kwa utaratibu, tayari vifaa vya maunganisho maya vimeshanunuliwa na wateja mtaanza kuunganishiwa hivi karibuni," Mhandisi Marryprisca amesema.

Tunampongeza sana Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uzalendo wake wa kutoa fedha za ahueni ya UVIKO 19 kiasi cha bilioni 2.5 kwenye mradi wa maendeleo ili wananchi wapate maji.

Mwakilishi wa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASAShaban Mkwanywe amesema anaishukuru Serikali kwa kuwezesha kutekeleza mradi huo na kuukamilisha.

Mradi huu umewezesha kujibu hoja za shida ya maji kwa wananchi, kwa sasa kazi inayoendelea ni kusambaza maji kwa wananchi

"Kwa mwaka huu wa fedha 2023/24 tumetenga fedha za ndani bilioni 2.5 kwa ajili ya kusambaza maji kwa wananchi wote wa kata ya Mbezi, Msakuzi kusini na kaskazini kuwa wasiwe na wasiwasi huduma itafika," Mhandisi Mkwanywe amesema.









Share To:

Post A Comment: