Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb)amechangisha kiasi cha shilingi  milioni 43 zitakazotumika kwa ajili ya ujenzi  wa Kituo  cha Mafunzo ya Wanawake, Watoto  na Vijana cha Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT)- Dayosisi ya Pwani huku matarajio ikiwa ni kupata milioni 200

Changizo hilo limefanyika leo Mkoani Morogoro ikiwa ni Siku ya sita ya kufunga Kongamano  la Wanawake wa Dayosisi ya Pwani.

Mhe.Masanja amesema Ujenzi wa kituo hicho utasaidia kuboresha maisha ya wanawake, watoto na vijana hivyo kuiunga mkono Serikali katika kukuza uchumi. 

"Ujenzi wa kituo hiki ni jitihada zenu za kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha hali ya maisha ya makundi haya katika kuwajengea uwezo na kukuza hali zao za kiuchumi na Taifa kwa ujumla".

Amefafanua kuwa kituo hicho kitakapokamilika kutaanzishwa  miradi mbalimbali  ambapo vikundi vya vijana na wanawake wataweza kupata  mikopo yenye masharti nafuu kutoka Halmashauri za Wilaya kwa ajili ya makundi hao ya wanawake na vijana 

Aidha, Mhe.Masanja amewapongeza Wanawake wa kongamano hilo kwa kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii kwa kutembelea Hifadhi ya Taifa Mikumi.

Naye Msaidizi wa Askofu, Mchungaji Amos Mlagwa amemshukuru Naibu Waziri Masanja kwa kujitolea kushiriki  kongamano hilo pamoja na kuchangisha fedha za ujenzi wa kituo  cha mafunzo ya wanawake, watoto na vijana.

Kauli mbiu ya Kongamano hilo ilikuwa ni  "Mwanamke mcha Mungu ni shupavu na jasiri".

Share To:

Post A Comment: