Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi amezindua kambi ya siku saba ya macho mtoto wa jicho kuanzia 22 septemba 2023 hadi 29 septemba 2023 inayofanyika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya.

Mahundi amesema yeye kama mwakilishi wa wananchi kiu yake ni kutafuta fursa kwa wadau ill kuhakikisha wananchi wanaimarika kiafya awali alitafuta wafadhili waligharamia matibabu bure kwa wagonjwa wa fistula.

Aidha amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyoelekeza fedha nyingi kwenye sekta ya afya nchini ukiwemo Mkoa wa Mbeya ambao nao umenufaika.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera amempongeza Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa namna anavyotekekeza shughuli za ujenzi wa Taifa.

Mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya Dkt Julius Kaijage ameishukuru serikali kwa kutoa fedha nyingi kwenye hospitali hiyo.

Baadhi ya wananchi wameshukuru kuletewa huduma hiyo kwani wengi hawawezi kumudu gharama za matibabu.


Share To:

Post A Comment: