𝗨𝘀𝗵𝗶𝗿𝗶𝗸𝗶𝘀𝗵𝘄𝗮𝗷𝗶 𝘄𝗮 𝗧𝗮𝗮𝘀𝗶𝘀𝗶 𝘇𝗮 𝗨𝗺𝗺𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗸𝘂𝗮𝗻𝗱𝗮𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗵𝘂𝗶𝘀𝗵𝗮 𝗩𝗶𝘄𝗮𝗻𝗴𝗼 𝗻𝗮 𝗠𝗶𝗼𝗻𝗴𝗼𝘇𝗼 𝘆𝗮 𝗦𝗲𝗿𝗶𝗸𝗮𝗹𝗶 𝗠𝘁𝗮𝗻𝗱𝗮𝗼

DODOMA.


Maafisa TEHAMA kutoka katika taasisi mbalimbali za umma wameshiriki katika kikao kazi cha kuandaa na kuhuisha Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao, ili kuhakikisha inaendana na Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019.  

Lengo ni kuhakikisha Serikali inakua na Serikali mtandao yenye tija na inayoongeza ufanisa katika utendaji kazi na utoaji huduma kwa umma.

Kikao hicho kilichoandaliwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), kilifanyika kwa siku 3 kuanzia Agosti 15, 2023 katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijijini Dodoma.
 

Viwango na Miongozo hiyo inapatikana katika Tovuti ya e-GA kupitia kiungo
https://www.ega.go.tz/standards
Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: