Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema serikali imetenga zaidi ya shilingi Bilioni hamsini na mbili kwa ajili ya ujenzi wa mradi mkubwa wa kuhifadhi maji taka Jijini  kupitia Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Mkoa wa Dar es Salaam(DAWASA) 

Akiongea eneo la Mbezi unakotekelezwa mradi huo Naibu Waziri wa Maji amesema mpaka sasa serikali imetoa shilngi bilioni saba kwa mkandarasi wa China malipo ya awali ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa utakaoondo changamoto ya maji taka Jijini Dar es Salaam ili maji hayo baada ya kufanyiwa matibabu yatumike kwenye matumizi mengine yakiwemo ya viwandani.

Mahundi amesema serikali pia imetekeleza miradi kama huo Jijini Dodoma na Arusha ambapo amezitaka Mamlaka zote nchini kubuni miradi kama hiyo.

Aidha Mahundi amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza fedha nyingi kwenye sekta ya maji hivyo Mamlaka zilizokuwa na miradi midogo midogo zihakikishe zinabuni miradi mikubwa kutokana na ukuaji wa miji nchini.

Mhandisi Shaban Mkonye kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa DAWASA amema mradi ukikamilika maji taka yakitibiwa yatatumika viwandani pia hata kunywa kwani teknolojia ya kutibu ipo.









Share To:

Post A Comment: