Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewapongeza madakitari na wauguzi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kutokana na juhudi mbalimbali zinazofanyika katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi huku akisisitiza weledi na uadilifu katika kazi.

Ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea na kukagua utoaji wa huduma katika Hospitali hiyo ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili Mkoani humo.

Waziri Ummy ameridhishwa na juhudi mbalimbali zinazofanywa na madakitari na wauguzi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga katika kuimarisha utoaji wa huduma bora huku akiwakumbusha kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na taratibu za wizara ya Afya.

“Nimefurahi kuona Hospitali hii kwa sasa inatoa huduma takribani kwa silimia  Mia moja hongereni sana kwenye hili nipongeze sana watumishi mmefanya kazi kubwa nimpongeza Dkt. Luzila na timu yako mmefanya kazi nzuri tena kwa ubunifu nisidanganye Shinyanga kwakweli nimefurahi na nimeridhika kwa asilimia Mia moja kama Waziri wenu niseme hamjamwangusha Rais Samia Suluhu Hassan”.amesema Waziri Ummy

Amesema mpango wa serikali ni kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa miundombinu yote muhimu katika Hospitali hiyo ikiwemo jingo la mama na mtoto pamoja na maabara.

Katika taarifa yake mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John amebainisha mafanikio, changamoto na mikakati mbalimbali ya Hospitali hiyo.

Kwa sasa huduma zote za matibabu ya wagongwa wa ndani na wagongwa wa nje zinafanyika katika Hospitali hii ya rufaa ikiwa ni pamoja na huduma zote za krinick za kibingwa zote, upasuaji watoto magongwa ya ndani  pamoja na watoto”.

“Kipaumbele chetu kwa sasa ni kujenga jingo la mama na mtoto, jengo la Maabara, Mochwari, Famasi na Laundry”.

‘”Uchache wa miundombinu za majengo ili kuweza kukidhi kutoa huduma zote katika Hospitali hii ni changamoto kwetu, kuna upungufu wa watumishi kwa asilimia 47, kuharibika kwa barabara na  kutokuwepo kwa Mochware hii nayo ni changamoto kubwa kwetu”.amesema Dkt. Luzila

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliopata huduma katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wamepongeza juhudi mbalimbali za uboreshaji wa huduma za Afya lakini wameiomba serikali ifanye juhudi za kuboresha barabara inayotoka mjini Shinyanga kuelekea Hospitali hiyo.

Aidha Waziri Ummy ameahidi kuendelea kushinikiza ili barabara hiyo iweze kuboreshwa katika kiwango cha lami ambapo amesema serikali itaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za Afya Nchini.

Naye  mganga mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile pamoja na mambo mengine ameahidi kuendelea kusimamia utoaji wa huduma za Afya.

Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu  emefanya ziara yake ya siku mbili Mkoa wa Shinyanga ambapo Alhamisi Julai 13,2023 ametembelea na kukagua utoaji wa huduma za Afya katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga na Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga huku akizungumza na watumishi pamoja na wananchi mkoani humo.

 Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu awali akiwasili Mkoani Shinyanga kwa ajili ya ziara yake ya kutembelea na kukagua utoaji wa huduma za Afya.


Share To:

Misalaba

Post A Comment: