DENIS CHAMBI, TANGA.

ZAIDI ya wanafunzi 60  wa shule za  sekondari kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wameshiriki kikamilifu  kongamano la saba la sayansi na Teknolojia lililoandaliwa na kituo cha sayansi Cha Stem Park chini project Inspire  wakifunzu na kuonyesha umahiri wao  katika  kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi kupitia sayansi  ,technolojia, uhandisi na hisabati.


Akifunga kongamano hilo la saba mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya jiji la Tanga Dr. Sipora Liana ameipongeza shirika la botna  foundation ambao ni wafadhili wa miradi mbalimbali inayotekelezwa jijini humo ikiwemo kituo cha Stem Park  huku walimu wanaowafundisha vijana na wanafunzi akiwataka mbali na elimu kuwafundisha pia maadili mema.

"Tunatambua mchango mkubwa sana wa botna foundation ni mengi sana wametusaidia katika nyanja ya kielimu kijamii na hata afya pia  wametoa Madawati ya shule za msingi Milion 286.3 , Mambo ya usalama barabarani wametoa million 442.5 , wamejengea uwezo kiuchumi vijana  million 434.9 hii miradi yote ni maendeleo makubwa ndani ya jiji la Tanga kwaajili ya wananchi" alisema Dkt. Liana

Akizungumza na wanafunzi hao amewataka kusimamia ndoto zao kujikita kimasomo zaidi kuhakikisha zinafanikiwa akiwataka kujiepusha na tamaa maswala ya ukatili ambayo yataweza kuharibu malengo yao  waliyojiwekea huku akiipongeza kituo cha Stem Park kwa uwezeshaji huo kwa vijana.

" jilindeni vijana  na  jitunzeni msome kwa bidii ili mfikie lengo wazazi wenu wafurahi na mtapata baraka nyingi kwa wazazi , mambo ya uzinzi , ukahaba ushoga , usagaji achaneni nayo zingatieni masomo yenu mfikie malengo yenu nawatakia kila la kheri" alisema Dkt. Liana

Mratibu wa makongamano hayo Dr. Isaya Ipyana  alisema kuwa  wanafunzi  hao ambao waliweka kambi kwa zaidi ya siku 5 katika kituo cha Stem Park wamekuwa wakiwaelekeza  namna gani ya kukabiliana na  changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi pindi wanapokuwa mashuleni na hata baada ya kumaliza elimu yao ambapo wataweza kutumia sayansi Teknolojia uhandisi na mahesabu ambayo walifundishwa kwa nadharia darasani na hivyo kufanya kwa vitendo hatua ambayo wakifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

"Kongamano la mwaka huu tulikuwa tumelenga hasa kwenye changamoto ya mabadiliko ya tabianchi jinsi gani ambavyo watatumia  sayansi uhandisi na mahesabu  kutatua changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwahiyo kuanzia tarehe 26 mpaka 30 June wanafunzi kutoka mkoa 10 ya Tanzania  nzima waliokuwa pamoja kukaa chini na kuutafuta njia mbadala  ambazo wanaweza kuzitumia " alisema 

" Wapo ambao waliweza kutengeneza ni ndege nyuki ( drones), wapo ambao waliweza kutengeneza  mitambo kwaajili ya gas, kwahiyo nia kubwa ni kuhakikisha Yale ambayo waliweza kujifunza darasani  kwa nadharia wajifunze kwa vitendo  hapa na  tunashukuru kwamba wamefanikiwa" alisema Ipyana. 

Alisema lengo lao kuu hasa ni kuwaandaa watoto na vijana ambao watakiwa Ni wabunifu  na kuweza kutatua changamoto mbalimbali kwa  kupitia yale amabayo walishayasoma darasani ikiwemo Yale ambayo yanawazunguka katika mazingira wanayoishi.

"Dhima kubwa Ni kuhakikisha tunatengeneza vijana  ambao ni wabunifu na kuweza kutatua changamoto mbalimbali  kwa kupitia Yale ambayo wanayasoma darasani  kwahiyo mafunzo haha yanahakikisha tunapata vijana wabunifu  ambapo pia Wana uwezo was kufikiria zaidi ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo tabia nchi  na zile ambazo zinawazunguka kwenye jamii yao" aliongeza Dk. Ipyana.

Akizungumza kwaniaba ya Botna Foundation Mbogolo Philoteus alisema shirika hilo linaamini kumuandaa kijana katika karne ya sasa na ijayo kwaajili ya kuingia kwenye soko la kiushindani hatua ambayo inasaidia kujiepusha kujiingiza katika mmomonyoko wa maadili na makundi maovu ambayo yanaweza kumfanya kutokutimiza ndoto zake kielimu , kijamii kisaiasa na nyanja mbalimbali. 

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki mafunzo hayo akiwemo  Nabiha Kassim na Innocent Richard wamekishukuru kituo cha Stem Park kwa elimu waliyoipata  ambayo mbali na kwenda kuitumia baada ya kumaliza masomo itakuwa ni fursa ya kuwatengenezea ajira ya baadaye.
 
 
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya jiji la Tanga Dkt. Sipora Liana akisikiliza maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya sekondari Philter Federal ya Zanzibar, Rashid Said kuhusu utambuzi wa mimea ikiwa ni njia moja wapo ya utunzaji wa mazingira na kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mwanafunzi Grace Daniel (kulia) akitoa maelezo  kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya jiji la Tanga Dkt.  Sipora Liana kuhusu kubaini usalama na hatari karibu na mazingira ya binadamu kutokana na mtambo walioutengeneza katika kituo cha sayansi cha Stem Park wakati wa maadhimisho ya wiki ya sayansi Afrika
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya jiji la Tanga Dkt. Sipora Liana akizungumza katika kongamano la saba la sayansi katika kituo cha sanyansi cha Stem Park june 30,2023 jijini Tanga.
Picha ta pamoja Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya jiji la Tanga Dkt. Sipora Liana akiwa na wanafunzi waliotunukiwa tuzo mbalimbali baada ya kufanya vizuri katika kongamano la saba la sayansi , kushoto kwake ni meneja wa kituo cha Stem Park Max George na kulia ni mwakilishi wa shirika la Botna Foundation Mbogolo Philoteus.
Mwakilishi wa shirika la Botna Foundation Mbogolo Philoteus akipanda mti katika maeneo ya kituo cha sayansi cha Stem Park kuashiria utunzaji wa mazingira ili kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi
Share To:

Post A Comment: