ROBERT Munisi kwa mara ingine tena ameibuka na ushindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani katika uchaguzi uliofanyika leo Julai 2 mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa KIBAFA, amesema amekuja kivingine ikiwa ni pamoja na kufanya mgawanyiko katika utendaji jambo ambalo imemlazimu kuunda Kamati mbalimbali ambazo zitakuwa tendaji katika masuala ya takayohusu KIBAFA, Kamati hizo ni pamoja na kuundwa kwa Bodi ya Wadhamini itakayoongozwa na Mwenyekiti wake Rugemalira Rutatina, Makamu Katibu ni OCD Mlandizi Julieth Lyimo Wajumbe ni Meja Jenerali Bahati na Mohammed Sumaye.
Aidha Munisi amezitaja Kamati zingine kuwa ni pamoja na Kamati ya Nidhamu na Maadili , Kamati itakayosimamia Soka la Vijana, Kamati ya Soka la Vijana na Wanawake,Kamati ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) pia amemtangaza Hassan Mtengefu kushika nafasi ya Meneja Habari wa KIBAFA.
Aidha nafasi ya Makamu Mwenyekiti KIBAFA imekwenda kwa David Mramba, Katibu Daudi Mhina na Katibu Msaidizi ni Omari Abdul Pumzi Mweka Hazina ni Laurent Didas
Naye Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani Mohammed Masenga ametoapongezi kwa KIBAFA kwa kufanya uchaguzi uliokuwa wa wazi na haki huku akitoa rai kwa wanachama kushirikiana vyema na uongozi ulioingia madarakani ipasavyo huku akisisitiza kuwa wawe na moyo wa kujitolea zaidi kwa sababu kazi ya mpira ni ya kujitolea zaidi na kuhakikisa soka Wilayani kibaha linakua na kuamsha hamasa zaidi kwa vijana.
Post A Comment: