Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amempongeza mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi kwa kutoa majiko ya gesi 600 ya kupikia kwa wajasiliamali wa Wilaya ya Shinyanga.

Ametoa pongezi hizo Ijumaa Julai 21,2023 akiwa mgeni rasmi kwenye hafla ya ugawaji majiko hayo ya gesi na kwamba hafla hiyo imekwenda sanjari na semina ya kutoa elimu ya matumizi Bora kwa wajasiliamali waliopokea majiko hayo.

RC Mndeme amesema majiko hayo yatawasaidia wananchi hao kuepukana na uchafuzi wa mazingira unaotokana na utumiaji wa kuni pamoja na mkaa wakati wa kupika.

“Asante sana Mhe. Mbunge kwa kutuletea majiko haya rafiki kwa mazingira, sasa tutapika kwa wakati mfupi na urembo wetu utaongezeka kwa sababu hatuchafuki tunakushukuru kwa kuwajali wananchi kata zote za Jimbo la Shinyanga na niwaombe muende  mkatumie majiko haya ya kisasa ili ndoa ziendelee kuimarika”.amesema Mndeme.

“Kati ya wabunge wanaofanya kazi vizuri, Katambi yumo Katambi ni kijana mchapakazi na msikivu sana, mlifanya maamuzi sahihi kumchagua mbunge huyu naomba tumuunge mkono, tusimkatishe tamaa, tumtie moyo na tumuunge mkono kwa kumpa ushirikiano, huyu ni mtoto wetu tusitafute mtoto mwingine”,amesema RC Mndeme.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Paschal Patrobas Katambi amesema ametoa majiko ya gesi zaidi ya mia tano yenye thamani ya Shilingi Milioni 20.

Amesema lengo la kutoa majiko hayo ni kuwaepusha wananchi na athari zitokanazo na matumizi ya mkaa pamoja na Kuni wakati wa kupika chakula ambapo amesema ataendelea kutoa majiko ya gesi kwa makundi mbalimbali ya wananchi katika jimbo lake.

“Nimefanikiwa kugawa majiko haya kwa neema ya Mungu kwa kushirikiana na Kampuni ya Oryx nimechukua mitungi zaidi ya Mia tano yenye thamani ya Shilingi Milioni 20 ili ikasaidie wananchi wa Shinyanga lakini natarajia pia kuja kugawa awamu ya pili kuweza kuhakikisha kwamba tunaunga mkono takwa la ilani ya chama cha mapinduzi la kuhakikisha tunatunza mazingira kwa kumtua mama kuni kichwani”.amesema Mhe. Katambi

Aidha Mhe. Katambi amemshukuru  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya  maji, elimu, afya, barabara na sekta zingine kwenye jimbo lake ya Shinyanga mjini.

Mhe. Katambi ametumia nafasi hiyo amewataka wananchi wa jimbo hilo kuwapuuza baadhi ya watu wanaopotosha kuwa Bandari ya Dar es salaam na Nchi imeuzwa ambapo amesema  serikali ina nia njema ya kufanya uwekezaji kwenye bandari ili kuongeza tija kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Baadhi ya wajasiliamali Wilaya ya Shinyanga waliopokea mitungi hiyo Wameshukuru huku wakiahidi kuitumia vizuri majiko hayo ili kuendelea kuwanufaisha.

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi  ametoa msaada wa Majiko 600 ya Gesi yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa wajasiriamali wakiwemo wauza kahawa, mama lishe na baba lishe pamoja na makundi mbalimbali ya wananchi katika jimbo hilo lenye jumla ya kata 17 kwa lengo la kuwaepusha wananchi na athari zitokanazo na matumizi ya mkaa pamoja na Kuni wakati wa kupika chakula huku akisema ataendelea kutoa majiko ya gesi kwa wananchi wake.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi akizungumza kwenye hafla yake ya kugawa majiko ya gesi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano jengo la CCM Mkoa wa Shinyanga.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi akizungumza kwenye hafla yake ya kugawa majiko ya gesi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano jengo la CCM Mkoa wa Shinyanga.

Hafla ya kukabidhi majiko ya gesi yaliyotolewa na mbunge wa jimbo la Shinyanga Mhe. Paschal Patrobas Katambi kwa wajasiliamali mbalimbali wakiwemo mama lishe, baba lishe na wauza kahawa ikiendelea katika ukumbi wa mikutano jengo la CCM Mkoa wa Shinyanga.






Share To:

Misalaba

Post A Comment: