Na ; Elizabeth Paulo,Dodoma 


Mkataba kati ya Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Pamoja na Benki ya NBC umetiliwa saini ukishuhudiwa na Waziri wa Elimu profesa. Mkenda kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa Vyuo vya Mamlaka ya Mafunzo na Elimu ya Ufundi(VETA) kupitia mradi wa wajibika Scholarship ambapo wanatoa sh.milioni 100 Kwa kuanzia huku Vijana 1000 wakinufaika na mradi huo.



Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Mkenda amesema pamoja na na fani zilizochaguliwa ambazo ni Ushonaji, useremala, Ufundi mechanical, ujenzi, pia iundwe timu maalum ambavyo itachangia fani moja itakayofundishwa ndani ya miaka 2 hadi mitatu ili kuleta ufanisi na kukuza soko la ajira kwa vijana hao.




Profesa.Mkenda ametoa maagizo hayo Julai 20,2023 jijini Dodoma, wakati wa hafla hiyo ya utiliaji saini baina ya Serikali ya Benki hiyo ya NBC.



Waziri Profesa. Mkenda amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuunda timu Maalum itakayo pita na kuangalia fani ambazo zinawigo mpana wa ajira.


"Mimi napendekeza iwe fani ya ushonaji na mitindo, kwa mfano nguo aina ya suti zinaagizwa kutoka nje ya nchi Kwa gharama kubwa na ni vazi ambalo linakubalika, hapa nchini wapo mafundi ambao wanakuja wanachukua vipimo wanapeleka nguo kushona nje ya nchi na gharama ni kubwa mana wateja wanalipa kwa dola,"amesema Prof.Mkenda.



Waziri huyo amesema wakipata wataalam katika eneo hilo ambalo lina wigo mpana wa ajira, watafanya vizuri na watapata fedha nyingi ambapo amewahakikishia uwazi katika matumizi ya fedha hizo kama wao walivyoomba na kwamba watakuwa huru kufanya ukaguzi wakati wowote watakapohitaji kufanya hivyo.


Awali Mkurugenzi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Theobald Sabi amesema uwepo wa changamoto ya soko la ajira ni suala la kidunia na vijana wengi wa Tanzania wanahangaika kutafuta ajira, kupitia changamoto hiyo NBC imeona umuhimu wa kuviwezesha vyuo vya VETA nchini kutoa elimu zinazotoa ajira Kwa vijana.




"Leo NBC inaungana na Serikali rasmi katika kuzindua ufadhili wa kuwasomesha wanafunzi wa VETA, kwa kuanzia NBC watawasomesha vijana 1000 katika vituo mbalimbali vya VETA nchini Kwa ufadhili wa milioni 100 Kwa kuanzia,"amesema Sabi



Amesema wanalenga kufadhili katika fani za ushonaji, mechanical, fundi ujezi na useremala, ambapo NBC itawaandikisha kwenye NBC business Class na kuwafungulia akaunti Maalum iitwayo NBC KUWANASI, ambapo wataweka Fedha na kutoa bila Makato yeyote na kupitia hapo wataunganishwa na fursa za kifedha kama mikopo ili kuendeleza shughuli zao.



Mkurugenzi huyo amesema mkopo wanaotoa utaratibiwa na wizara na VETA, Benki inasisitiza kuwa mshirika wa Serikali katika kuendeleza elimu nchini.



Naye Kaimu Mkurugenzi VETA, Anthony Kasore, ameishukuru NBC huku akiwathibitishia kuwa watahakikisha vijana wa kitanzania wanaenda kupata ujuzi.




"Katika hili nipende kumshukuru Rais Samia ambaye anahitaji kuona vijana wakipata ujuzi wa mafunzo ya amali hapa nchini, tumepokea Fedha hizo Kwa ajili ya kwenda kutekeleza ujuzi ambao vijana wengi wanahitaji, vijana wengi wanahitaji ajira lakini wanakosa ujuzi,"amesema.





Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: