Na Dotto Mwaibale, Singida

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Singida, Martha Mlata (pichani) kesho Julai 3, 2023, anatarajia kuwasha moto wakati atakapo kuwa katika ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Singida ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara hiyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Singida Shabani Hamisi alisema ziara hiyo katika wilaya hiyo ni ya muhimu sana kwao.

"Ziara hii aatakayoianza kesho mwenyekiti wetu wa chama mkoani hapa ni ya muhimu sana kwa ajili ya kukihimarisha chama," alisema Hamisi.

Akizungumzia mambo atakayoyafanya wakati wa ziara hiyo alisema atatembelea Balozi Shina namba tisa lililopo Kitongoji cha Mnung'una ambapo pia atapata fursa ya kuzungumza na wananchi wakiwemo Wana CCM na kupata taarifa ya chama.

Alisema kazi nyingine ambayo ataifanya ni kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo na moja ya miradi hiyo ni ujenzi wa shule za Boost uliopo  Kata ya Minga na ujenzi wa Barabara ya kiwango cha lami na kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kata hiyo.

Hamisi alisema katika ziara hiyo Mlata ataongozwa na wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya hiyo chini ya Mwenyekiti Lusia Mwiru.

Mwenyekiti huyo wa chama mkoani hapa Martha Mlata ataendelea na ziara hiyo katika wilaya ya Mkalama atakayoifanya Julai 4, 2023, Iramba, Julai 5, Ikungi Julai, 6, Singida Vijijini, Julai 7 na kumalizia katika Wilaya ya  Manyoni Julia 8 na 9.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: