DENIS CHAMBI, TANGA.
WAZIRI wa Afya na mbunge wa jimbo la Tanga mjini Ummy Mwalimu amesema kuwa amejiapanga kulitangaza jiji hilo kupitia mazao yatokanayo na Bahari na kuzidi kuwavutia wawekezaji ambao watasaidia kukuza uchumi wa wananchi na hatimaye kuchangia pato la Taifa kwa ujumla.
Ummy amesema hayo leo July 17 katika ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali iliyopo chini ya taasisi Tanga yetu ambayo inafadhiliwa na Botner foundation ambao wamewekeza jumla ya shilingi Billion 7 kwa awamu ya kwanza katika sekta ya uvuvi hususani kilimo cha Mwani, kunenepesha kaa, kuwawezesha vijana kiuchumi.
"Kwa niaba ya wakazi wa jiji la Tanga tunapenda kuwashukuru na kuwapongeza sana kwa kuunga mkono jitihada za serikali kuboresha miundombinu kwa wakazi wa jiji la Tanga hususani kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi katika miradi ya uvuvi, kuwawezesha vijana katika kilimo, ufugaji wa kuku na samaki pamoja na kuboresha eneo la Bustani ya Forodhani haya ndio maendeleo ambayo tunataka kuyaona katika jiji letu la Tanga"
"Tunataka kuufanya mwambao wa Tanga kuwa ndio kinara cha uzalishaji wa mazao ya Bahari hususani mazao ya Mwani, Majongoo Bahari pamoja na Kaa tunachotaka sasa hivi ni kutafuta wadau wengi zaidi watusaidie kuwekeza zaidi" alisema Ummy
Amesema kuwa ataendelea kudumisha mahusiano na wadau mbalimbali chini ya wizara ya mifugo na uvuvi ili kuendeleaza mazao yatokanayo na Bahari huku akiwavutia wawekezaji wengi zaidi kuja kuwekeza kwa lengo la kuendelea kutangaza Tanga.
"Nawashukuru sana Botner foundation kwa juhudi wanazoendelea kufanya na kuunga mkono lakini tunahitaji kuboresha ubia zaidi kwaajili ya kuboresha maisha ya wakazi wa jiji la Tanga, kwa kweli tunapaswa kulikumbatia zao la Mwani ni zao lenye faida kubwa tutashirikiana na Botner foundation chini ya wizara ya mifugo na uvuvi kuhakikisha tunaendeleza kilimo Cha zao la Mwani kwanza kabisa kuwapa elimu na ujuzi wananchi". alisema Ummy.
Akizungumza mwakilishi wa shirika la Botner foundation Dkt Hassan Mshinda amesema kwa awamu hii ya kwanza wamefadhili miradi mbalimbali inayotekelzwa ndani ya jiji la Tanga ikiwa na zaidi ya shilingi Billion 7.
"Tunashukuru sana kwa ushirikiano tunaoendelea kuupata kutoka kwa halmashauri ya jiji na mbunge wetu Ummy Mwalimu , hii ni kazi iliyofanywa kwa muda wa miaka miwili na nusu lakini tunategemea kwamba tutaweza kuendelea kwa muda mwingi zaidi na miradi mingine mingi ambayo inalenga kuwasaidia zaidi vijana kuwewezesha kiuvumi" alisema Dkt. Mshinda.
Kwa upande wake Afisa uvuvi ambaye ni msimamizi wa mradi wa uvuvi kupitia miradi ya Tanga yetu Omari Mohammed amesema kuwa kumekuwa na mabadiliko chanya kwa wananchi wanotekeleza miradi hiyo ambayo imekuwa ikiwaapia kipato ikiwemo unenepeshaji wa kaa, kilimo cha Mwani, ufugaji wa samaki wa sato.
Wakizungumza katika ziara hiyo baadhi ya wavuvi akiwemo Khatibu Enzi wameeleza changamoto ya uvuvi haram sambamba na kuibiwa vifaa vyao ikiwemo ngalawa na kuchomewa boti wakiiomba serikali kuwasaidia kuimarisha ulinzi na usalama na kufanya doria za mara kwa mara .
"Ndani ya miezi mitatu sasa vyombo vyetu Kama tisa vimepotea na hii hali imekuwa ukitokea kama doria lakini doria hiyo haina taarifa kwenye serikali za mitaa au ofisi za mazingira kwahiyo vyombo vikipotea tukivitaguta havijulikani vikowapi hiyo imekuwa Ni changamoto kubwa sana kwetu sisi wavuvi" alisema Enzi.
Post A Comment: