Waendesha boda boda wa Kata ya Mwankoko katika Manispaa ya Singida wakiongoza msafara wa Mbunge wa Singida mjini Musa Sima alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo na kufanya mkutano wa hadhara ambao pia alipata fursa ya  kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi kwenye mkutano uliofanyika kata hiyo, Julai 17, 2023.

..............................................................................


Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUNGE  wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima amewatoa hofu wananchi wa jimbo hilo na Mkoa wa Singida kwa ujumla kuhusu mkataba wa uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam na kueleza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amekuwa na nia njema kuhusu jambo hilo.

Sima ameyasema hayo jana Julai 17, 2023 wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya  Mwankoko katika mkutano wa hadhara wakati wa siku yake ya pili tangu aanze ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika kata hiyo.

Alisema kumekuwa na upotoshaji mkubwa juu ya uwekezaji wa bandari  ya Dar es Salaam kutoka kwa baadhi ya watu ambao hawaitakii mema nchi yetu jambo ambalo sio zuri hata kidogo na wana Mwankoko wanapaswa kuelewa.

"Sisi kwenye sera yetu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM ) tunazungumzia uwekezaji hatuzungumzii ubinafusishaji lakini wale wasiotutakia mema na Rais wetu na nchi yetu wameanzisha upotoshaji mkubwa sana ambao tusipokuwa makini unaweza kutugawanya..

Alisema bajeti ya Serikali iliyopitishwa hivi karibuni ni Sh.Trilioni 44 katika fedha hizo trioni 10 ni mishahara ya wafanyakazi, trilioni 16 zinalipa madeni ya nje  na zinabaki trilioni 18 ndizo zinazotumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema anataka kuwaonesha mzigo mkubwa ambao Rais Samia ameubeba na Serikali kwa fedha hizo kuzigawanya katika Halmashauri ambazo hazipungui 185,000 zote zinahitaji huduma mbambali zikiwemo za afya, elimu na vitu vingine vyote ambapo fedha hizo ni ndogo.

Alisema jambo  la kushangaza ni pale anakuja mwekezaji kuwekeza kwenye eneo hilo ambalo tunapata fedha ndogo ambazo hatuwezi kuzilinganisha na uwekeza uliopo katika bandari hiyo ambayo taarifa zake kila mwaka zinaeleza tunakusanya Sh.Trilioni 7 tu.

"Sasa tulipopata mwekezaji huyu  sisi kama wabunge tulihoji maswali baada ya uwekezaji huyo tutapata shilingi ngapi ambapo tuliambiwa tutapata Trilioni 26 ambazo ni nusu ya bajeti ya nchi iliyopitishwa ambapo Bunge liliridhia mkataba huo kwa kuzingatia sheria ya uwekezaji huo na ilipendekezwa kampuni hiyo ya DP World isajiliwe Brela hapa nchini na wao wataingia mkataba na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) jambo ambalo litasaidia kusitisha mkataba huo kwa sheria zetu iwapo watashindwa kutimiza masharti.

Katika mkutano huo  Mbunge alitoa fursa kwa wananchi kuuliza maswali mbalimbali ambayo yalihusu changamoto tofauti tofauti ambazo zilijibiwa na wataalamu  kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA),Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mjini Singida (SUWASA).

Mbunge Sima akiwa ameongoza na wajumbe wa kamati ya Siasa ya Wilaya ya Singida alikagua miradi mbali mbali iliyotekelezwa Kata ya Mwankoko ikiwepo Shule Shikizi ya Mwachichi,Zahanati ya Mtaa wa Isomia na Mradi wa Umeme wa REA unaoendelea kutekelezwa kwenye kata hiyo ambapo wananchi wataunganishiwa kwa gharama ya Sh.27,000 tu.

Aidha, Mbunge Sima alizungumzia changamoto ya malipo ya Wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) yakufuata fedha za malipo yao benki ambapo alisema aliomba kuwekwa mawakala ambao watakuwepo katika kata jambo litakalo saidia kuondoa adha waliyokuwa wakiipata kupata fedha hizo.

Changamoto nyingine iliyojiri kwenye mkutano huo ni ile ya kuanzishwa kwa bwawa la maji taka katika eneo hilo ambalo imedaiwa limekuwa likitoa harufu kali na kujaa kwa inzi hivyo kuhatarisha usalama kwa wananchi wanaoishi jirani na bwawa hilo ambapo waliomba wahusika waliondoe au wapewe fidia ili waweze kuhama.

Wananchi wa kata hiyo  walimshukuru Mbunge Sima kwa jinsi anavyoshirikiana nao na kujitoa kwake kuwasadia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa Zahanati ya Mtaa wa Isomia ambayo aliianzisha kwa kutoa Sh.Milioni 2 na Unyianga ambazo zinakwenda kutoa huduma kwa wananchi wa maeneo hayo hasa kwa mama na watoto ambapo waliamua kumzawadia zawadi ya mbuzi jike.

Leo Mbunge Sima ataendelea za ziara yake kwa kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata ya Unyianga na kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara akiongozwa na Diwani wa Kata hiyo, Geofrey Mdama

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima,akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Kata ya Mwankoko.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima, akipata maelezo kutoka kwa mkandarasi ambaye amejenga vyoo vya Shule Shikizi ya Mwachichi.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima akipongezwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Isomia Omari Ramadhan Muna kwa kujitoa kwake kuwasaidia wananchi wa kata hiyo katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hapo ni baada ya kukagua Zahanati ya Mtaa wa Isomia ambayo kwa kiasi kikubwa mchanga wake wa fedha ndio umesaidia kukamilisha ujenzi akiwa kama mwanzilishi wa ujenzi huo.

Viongozi na Wananchi wa Kata ya Mwankoko wakimzawadia mbuzi jike Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini kutokana na mchango wake mkubwa katika kuwafanikishia miradi mbalimbali ya maendeleo.
Msafara wa bodaboda ukiongoza magari katika ziara hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima, akipata maelezo kutoka kwa wataalam wa TANESCO wakati wakimpa taarifa ya utekelezaji wa Umeme wa REA katika kata hiyo.

Diwani wa Kata ya Mwankoko, Emmanuel Madaki, akizungumzia miradi mbalimbali iliyotekelezwa kwenye kata hiyo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mwankoko, Yahaya Njoghomi akizungumza katika mkutano huo wa hadhara.

Ukaguzi wa ujenzi wa vyoo katika Shule Shikizi ya Mwachichi ukifanyika.
Maelezo yakitolewa wakati wa ukaguzi wa Shule Shikizi ya Mwachichi.
Muonekano wa Zahanati ya Mtaa wa Isomia baada ya ujenzi wake kufikia hatua za mwisho.
Ukaguzi wa ujenzi wa choo cha Zahanati hiyo ukifanyika.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima akizungumza na wnanchi baada ya kukagua ujenzi wa Zahanati hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima akilakiwa  baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara.

Kwaya ikitoa burudani.
Mhandisi Beatus Samuel msimamizi wa utekelezaji wa umeme wa REA katika kata hiyo akijibu maswali ya wananchi kuhusu mradi huo.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima, akiwasalimia wazee waliofika kwenye mkutano huo.
Wanawake wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanakwaya ya Samaria wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Burudani za nyimbo za utamaduni wa kabila la Wanyaturu zikiimbwa.
Mserebuko ukifanyika kwenye mkutano huo.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mwankoko, Yahaya Njoghomi, akicheza sanjari na Msanii wa Kata hiyo.
Wanafunzi nao walikuwepo kumsikiliza mbunge wao kipenzi baada ya kutoka shule.
Kwaya ya Samaria ikitoa burudani.
Burudani ikitolewa na Kwaya ya Samaria.
Taswira ya mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwankoko A, Jacobo Yohana, akifungua mkutano huo.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mwankoko, Habiba Ryakuka , akiongoza mkutano huo.
Aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Isomia, Samson Samweli, ambaye sasa amepandishwa cheo na kuwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Unyambwa baada ya kufanya kazi iliyotukuka ya kusimamia ujenzi wa Zahanati ya Mtaa wa Isomia akiwaaga rasmi wananchi wa mtaa huo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Kata ya Mwankoko, Tumaini Jackson, akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu wa CCM wa Kata ya Mwankoko, Daud Muna , akizungumza kwenye mkutano huo.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa wa Wilaya ya Singida, Hawa Ntandu, akizungumza.
Mkutano ukiendelea,
Mjumbe wa kamati ya siasa wa Wilaya ya Singida, Ramadhani Mtipa, akichangia jambo kwenye mkutano huo wakati akijitambulisha.

Maafisa kutoka SUWASA nao walikuwepo kwenye mkutano huo kwaajili ya kujibu maswali ya wananchi yaliyohusu changamoto ya maji.  Kushoto ni Mhandisi Elisha Kivuyo na Neema ambaye ni Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja SUWASA Mkoa wa Singida.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: