Na John Walter- Babati

Mbunge wa jimbo la Babati Mjini Paulina Gekul (Naibu waziri wa katiba na Sheria) amewataka wasimamizi wa pesa za serikali zinazotolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya elimu kusimamia ipasavyo na kuikamilisha kwa wakati na ubora unaotakiwa.

Amezungumza hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo katika shule ya Sekondari Babati day panapojengwa Bwalo ambapo Milioni 50 imetolewa kwa ajili ya kumalizia ujenzi. 

Amesema Serikali inaendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya elimu na fedha za miradi mbalimbali ukiwemo wa BOOST kuboresha elimu ya msingi na sekondari kuongeza fursa ya upatikanaji wa elimu ili kupunguza vikwazo vinavyosababisha wanafunzi kuacha shule na kupunguza changamoto za upatikanaji wa elimu nchini.

"Serikali ipo Makini kufuatilia kila hatua ya utekelezaji wa miradi na haitasita kumuajibisha atakaekwenda kinyume" alisisitiza Gekul

Jengo hilo linatajwa kukamilika ifikapo Julai 20/2023.

Miradi mingine aliyotembelea Mbunge ni shule za Msingi Kwaang',  Komoto na Nakwa ambazo zimepokea shilingi milioni 81.3 kila moja kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu na matundu matatu ya vyoo.

Hata hivyo ujenzi wa Madarasa hayo shule ya Msingi Nakwa umekamilika huku Komoto na Kwaang' wakitarajia kukamilisha Julai 20 mwaka huu na yote yapo hatua ya upauzi pamoja na vyoo.

Mkuu wa shule ya msingi Kwaang' Mwalimu Iddy  Maje amesema madarasa hayo yatakapokamilika yatasaidia kupunguza msongamano mkubwa wa Wanafunzi na Kufanya Mazingira ya kufundishia kuwa rafiki.


Share To:

Post A Comment: