Na John Walter-Babati

Mbunge wa jimbo la Babati Vijiji  Daniel Sillo ameendelea na ziara  katika jimbo lake  kusililiza Kero za wananchi katika kijiji cha Utwari kikiwa ni kijiji cha 74 kati ya 102 vya jimbo hilo.

Wakizungumza  baadhi ya wananchi hao akiwemo Rosemery Antoni, ameipongeza serikali kwa kuimarisha miundombinu ya elimu na bara bara ikiwemo kukamilika kwa daraja la Yassi pamoja na miradi mingine katika sekta ya ya afya huku akiiomba serikali kuharakisha mradi wa maji wa ziwa Madunga ili kumaliza changamoto ya uhaba wa maji katika maeneo yao.

Naye Joshua Nada Mkazi wa kijiji cha Utwari ameiomba serikali kuanzisha miradi ya Umwagiliaji hasa katika kilimo cha Vitunguu katika kijiji cha Utwari ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Kwa upande wake Mbunge wa Babati Vijijini Mheshimiwa Daniel Sillo  amesema ataendelea kusimamia miradi ya serikali na kuwasemea wananchi katika mambo mbalimbali ukiwemo mradi wa ziwa Madunga ambao utamaliza changamoto ya maji katika kata 6 za ukanda wa juu Utakaogharimy shilingi Bilioni 6.

Aidha Sambamba na hayo Mhe. Daniel Sillo ameahidi Kuchangia Mifuko 50 ya Saruji  kumaliza Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu katika shule ya Sekondari Utwari iliyopo kata ya Madunga.

Kwa upande mwingine  Sillo amewapongeza wananchi wa kata ya Madunga kwa kushiriki katika ujenzi wa kituo cha Afya kilichogharimu shilingi Milioni 500.

Share To:

Post A Comment: