Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mwenyekiti wa kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi ameikumbusha jamii kutoa taarifa za ukatili ikiwemo ubakaji, ulawiti pamoja na ndoa za utotoni.

Ameyasema hayo akiwa mgeni rasmi katika bonanza la kupinga ukatili Cheupe Cup ambao limefanyika kwa siku sita mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga na kwamba bonanza hilo limekwenda sanjari na michezo mbalimbali katika uwanja wa Balina English Medium primary school.

Madam Kisendi pamoja na mambo mengine ameisihi jamii kupaza sauti juu ya ukatili kwa kutoa taarifa za vitendo hivyo ili hatua zaidi ziweze kuchukulia na serikali.

Amewasisitiza watoto kutoa taarifa za ukatili unaofanyika shuleni huku akiwaomba wazazi na walezi kujenga tabia ya kuzungumza na watoto baada ya kutoa shule ikiwa ni pamoja na kuwakagua kwa lengo la kuimarisha usalama wao.

“Pamoja na kwamba mtaa wa Dome uko vizuri kiutendaji lakini upo ukatili unaoendelea kufanya katika eneo hili, sasa hivi kuna janga kubwa linaendelea katika Mkoa wetu wa Shinyanga ukatili wa kimwili hasa watoto kubakwa na wengine kulawitiwa na haya yote uzembe unaanzia kwenye familia zetu wazazi kaeni vizuri na watoto wenu msiwatelekeze hakikisheni wanapata haki zao sasa hivi watoto kesho wanafungua shule kwanza mtoto usikubali kushikwa shikwa au kupewa zawadi na mtu usiyemfahamu mwisho wake atakukatili”.amesema Mwenyekiti Madam Kisendi

“Sisi SMAUJATA tupo kwa ajili ya kuibua ukatili unaofanyika kwahiyo mtu yoyote na wewe mtoto ukifanyiwa ukatili toa taarifa usikae kimya akiwa mama na baba zetu kuna vitu vibaya vinafanyika huko kwenye jamii paza sauti tupeni taarifa sisi tutawatetea kumbuka ukatili unarudisha nyuma maendeleo upo ukatili wa kimgono unafanyika, ukatili wa kiuchumi lakini pia zipo mimba za utotoni madhara yake ni makubwa husababisha vifo kuwa makini epuka kufanyiwa ukatili epuka kufanya ukatili”.amesema Madam Kisendi

“Akina mama tuwe walezi wa watoto wetu hakikisha mtoto yoko salama anapocheza, anapotoka shule mkague  niwaombe sisi sote tuliohudhuria hapa tukawe mabalozi wazuri kwa wengine mkawaambie watoe taarifa za ukatili SMAUJATA tutazipokea na kuzifikisha sehemu husika”.amesema Madam Kisendi

Kwa upande Afisa ustawi wa jamii Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Bwana Leopald Hamza ameeleza hatua mbalimbali za kufanya baada ya kubaini vitendo vya ukatili katika jamii.

“wengi wanapokumbana na masuala ya ukatili hawajui nini cha kufanya wengi wamekuwa wakiondoa ushahidi unakuta mtoto amebakwa au amelawitiwa mzazi hajui nini cha kufanya anamuogesha au anambadilishia nguo mtoto unapokutana na mtoto kafanyiwa tukio hilo usibadilishe kitu chochote wala usimuogeshe kitu cha kwanza nenda kwa mtendaji wako au mwenyekiti au dawati la polisi au kwa afisa ustawi wa jamii au ripoti kwa hawa SMAUJATA ili uweze kupata msaada wa haraka na sisi tutakuunganisha na madakitari kwa uchunguzi zaidi ukiwa na vielelezo vya ushahidi ambavyo vitatusaidia sisi kuweze kushinda kesi”.amesema Afisa ustawi Hamza

Viongozi mbalimbali wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wametoa elimu ya ukatili huko baada ya wananchi waliohudhuria bonanza hilo wakiipongeza kampeni ya SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa elimu hiyo ambapo wameahidi kuendelea kutoa taarifa za ukatili unaoendelea kufanyika katika jamii.

 

Mgeni rasmi Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi na viongozi mbalimbali wakiwa katika zoezi la kukagua timu za mpira leo Jumapili Julai 2,2023 katika uwanja wa Balina English Medium primary school mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.



Share To:

Misalaba

Post A Comment: