Mwenyekiti wa UVCCM Babati Mjini Ndg MAGDALENA URONO ahitimisha mafunzo ya mradi wa kukuza ajira na ujuzi kwa maendeleo ya Afrika (E4D) kwa awamu ya tatu na kuwatunuku vyeti vijana wapatao 189 katika chuo cha VETA Manyara.

Ndg Magdalena amemshukuru Mhe Rais DKT SAMIA SULUHU kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutengeneza mazingira rafiki ili vijana waweze kujiajiri.

Aidha ameyashukuru mashirika ya kimataifa GIZ, NORAD, KOIKA na EU kwa kufadhili mradi huu kwa kushirikiana na ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Aliwaasa vijana kutumia vyema fursa ya ujuzi walioupata katika kujikwamua kiuchumi

Aliwataka wale vijana ambao hawatapata ajira katika sekta rasmi kutengeneza vikundi ili waweze kuaminika hatimaye kupata mikopo kutoka katika sekta mbalimbali za kifedha

Mwisho, ameushukuru uongozi wa VETA Manyara chini ya Kaimu Mkuu wa Chuo Ndg, GULNAT NZOWA kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwapa ujuzi vijana. 
    
Share To:

Post A Comment: