Vijana zaidi ya 140 Kutoka Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Kutoka Mikoa takribani 8 ya Tanzania Bara Wamekusanyika Mkoani Njombe kwa Muda wa Mwezi Mmoja ili Kupata Mafunzo ya Ukarabati na Matengenezo ya Barabara kwa Kutumia Teknolijia stahiki ya Nguvu kazi ili Kuwafungulia Milango ya Fursa katika Mikoa yao.


Akizungumza na Vyombo vya Habari Mwenyekiti wa Jumuiya Hiyo ya Vijana UVCCM Mkoa wa Njombe Samweli Mgaya amesema kuwa lengo la Kuwaleta Pamoja Vijana Hao Kutoka Mikoa nane ya Tanzania bara ni kutaka  kuwapa Uzoefu na Ujuzi wa kazi mbalimbali kama Vile Ukarabati wa Barabara ambazo wanaweza kuzifanya katika Maeneo yao na Hivyo kuwa na Uwezo wa Kujiongezea Kipato na Kujiimarisha Kiuchumi,Hivyo sisi Vijana Tunachokiomba Kutoka kwa Serikali na kwa Rais kwamba Sisi Vijana Tumesoma Mfunzo haya na Tuko tayari kuunda Vikundi pamoja na Kufungua Kampuni ndogo kwaajiri ya Kumsaidia Katika Kazi mbalimbali kama Hizi za Ukarabati na Matengenezo ya Barabara.


"Mafunzo haya Tumeyaendesha Mkoa wa Njombe na Tumeyaratibu kwa Kushirikiana na Mkoa wa Singida,katavi,Rukwa,Songwe,Mbeya,Iringa,Mtwara na Njombe yenyewe ambapo tunaambiwa Mafunzo haya yanauwezo wa kufanya mtu aweze kukarabati barabara za Changalawe na hata Barabara za Tanroads,Hivyo tunaamini kupitia mafunzo haya Tunauwezo wa kufanya kazi na Taasisi mbili za Tanroads na Tarura"Samweli Mgaya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe


Donatha Kamwela ni Mkufunzi kutoka Taasisi ya Teknolijia ya Ujenzi ambayo inatoa  Mafunzo ya Ukarabati na Matengenezo ya Barabara kwa Kutumia Teknolojia Stahiki ya Nguvu kazi kwa Vikundi vya Wanawake na Vijana ambayo iko Chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi amesema baada ya Kutoa Mafunzo hayo kwa takribani Wiki nne anaamini Vijana Wameiva na Sasa Wapo tayari Kutumia Fursa zinazotangazwa na Taasisi za Serikali kama Vile Tanroads Pamoja na Tarura.


"baada ya Kutoa Mafunzo haya nimeona utayariwa Vijana kwani wanaonyesha Shauku ya kubwa ya Kuendelea Kujifunza lakini wapo kwaajiri ya kwenda kutekeleza Miradi mbalimbali ya matengenezo ya Barabara"


Neema Sigala ndiye Mratibu wa Mafunzo hayo hapa anawaomba Viongozi wa Mikoa Husika walipotoka Vijana hao kuwapa Fursa Mbalimbali kulingana na Mafunzo Waliyoyapa Huku Rebecca Julius Welia Pamoja na Godson Kaijage Wakipongeza Jitihada za Viongozi wa UVCCM Kwa Kuwapa Fursa Hizo.


Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Njombe bwana Samweli Mgaya ambapo Vijana kutoka Mikoa ya Kusini Wameweka kambi Mkoa wa Njombe kwaajiri ya Kujifunza Fursa mbalimbali za Ukarabati na Matengeenezo ya Barabara.

Share To:

Post A Comment: