Naibu Mkurugezi Mtendaji wa Usambazaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania Mhandisi Athanasius Nangali,akizungumza.


MENEJA wa Shirika la Umeme Tanzania TANECO, Mkoa wa wa Dodoma Mhandisi Donasiano Shamba amewataka wafanyakazi wa Shirika hilo kuzingatia mazoezi ili kuimarisha afya zao ili kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa wananchi.


Shamba ameyasema hayo jijini hapa wakati wa Bonanza la michezo lilohudhuriwa na wafanyakazi wa Shirika hilo ambapo pamoja na kushiriki michezo mbalimbali, wafanyakazi hao wamehimizwa kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa wananchi.


"Kama Mkoa wa Dodoma tutaendelea kusimamia utendaji kuhakikisha huduma bora zaidi kwa Wateja wetu kwa kuhakikisha tunachochea na kusimamia vizuri afya za wafanyakazi haswa kupitia michezo ambayo ni kipaumbele katika kuhakikisha tunafanikiwa." Alisema Shamba.


Bonanza hilo limefanyika kwa kushirikiana na benki ya Biashara ya Akiba ambapo Mshindi wa Jumla ilikuwa ni timu ya mpira wa miguu ya Dodoma Mjini iliyowachapa timu ya Chamwino kwa magoli matatu kwa mawili na kuondoa na kombe la Bonanza.


Pia katika hafla fupi ya jioni iliyoambatana na Bonanza hilo, TANESCO kupitia Naibu Mkurugenzi wa Usambazaji Mhandisi, Athanasius Nangali ilitambua Wateja wake vinara Mkoa wa Dodoma ambao ni DUWASA na UDOM pamoja na CFM Radio kama mdau maalum kwa Shirika.

Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: