Na; Elizabeth Paulo, Dodoma 

IDARA ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji, Serikali Kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, ina jukumu kubwa la kusimamia, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa sera, mipango, programu, miradi na mikakati mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Serikali.

Hayo yamesemwa leo 9 June 2023, na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga alipofungua mkutano wa wadau wa maendeleo ambao pamoja na mambo mengine, ulijadili swala zima la tathmini na ufuatiliaji wa shughuli za Serikali pamoja na kongamsno la wiki ya Ufuatiliaji, Tathmini na mafunzo itakayofanyika mapema mwezi Septemba mwaka huu.

Mhe. Nderianaga amesema  kuanzia sasa  Taarifa ya Serikali ya utendaji ya kila Mwaka itakuwa ikisomwa bungeni ili wananchi kuweza kufahamu utendaji wa serikali na kutoa taswira halisi ya uwajibikaji wa Serikali kwa wananchi.

Baada ya Serikali kufanya maboresho ya Muundo wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) 2022/23, Idara hiyo mpya iliyoanzishwa, ndiyo inahusika moja kwa moja na kuandaa taarifa za utendaji wa Serikali za kila robo mwaka, nusu mwaka na taarifa za mwaka ikiwemo taarifa za utekelezaji wa miradi inayotekelezwa ndani ya Taasisi za Umma na utekelezaji wa Malengo ya kimataifa na kikanda pamoja na  Ajenda ya Maendeleo ya Afrika. 

“Taarifa hizi, zitaonesha mwenendo na mwelekeo katika utendaji wa majukumu ya taasisi zote za Umma zikiwemo Wizara, Idara za Serikali zinazojitengemea, Wakala za Serikali, Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa”. Alisisistiza Naibu Waziri.


Aidha, Naibu Waziri ameendelea kusema kuwa ,Taarifa ya mwaka ya utendaji wa Serikali itakuwa ikisomwa Bungeni kuanzia mwaka ujao wa fedha (2023/24) ili kutoa taswira halisi ya uwazi na uwajibikaji wa Taasisi zote za Serikali kwa Wananchi.

 “ili kuwezesha Ofisi kupata taarifa hizi, itakuwa inafanya ufuatiliaji wa mara kwa mara wa viashiria vya utendaji kazi na kutoa taarifa katika ngazi mbalimbali.” Alifafanua

Awali, Naibu Waziri Nderiananga alisema kuwa Ofisi hiyo ipo maandalizi ya Kongamano la Pili la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 12 – 15 Septemba, 2023 Mkoani Arusha, Kongamano ambalo litawaleta pamoja, wadau wa maendeleo wa ufuatiliaji na tathmini ya Utendaji kazi ili kupashana habari na kupeana uzoefu wa namna ya kusimamia utekelezaji wa mipango, programu na miradi mbalimbali na kuonesha namna inavyosaidia jamii.


Akizungumza kwaniaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera Bunge na uratibu,Eliuter Kiwhele ambaye ni Mkurugenzi wa Mipango na Bajeti wa Ofisi yan Waziri Mkuu amesema kuwa wanaimarisha ufuatiliaji na tathmini hivyo kikao hicho ni muhimu ili kuweka malengo ya tahmini na Sera.

Kwa upande wake John Bosco Kaimu Mkurugenzi Idara ya ufuatiliaji na tathmini ya utendaji wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu amesema kuwa Wanafanya tathmini ya uwezo wa wataalam ili kujua maeneo yanayohitaji kuimarishwa ili kuunda mpango wa ufuatiliaji ngazi ya Taasisi za serikali






Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: