Na;Elizabeth Paulo, Dodoma 

Rai imetolewa kwa Wafanyabiashara na Watanzania kwa ujumla kuunga mkono juhudi za Serikali katika uwekezaji wa bandari ya Dar es salaam.


Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Mbunge wa Geita Vijiini Joseph Musukuma wakati akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu mjadala mkubwa umaoendelea nchini wa mkataba wamashirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu Bandari ya Dar es Salaam.Musukuma amewataka watanzania kutoyumbishwa na maneno ya watu wasioitakia mema nchi bali wamuunge mkono Rais kwenye uwekezaji wa bandari ya Dar es salaam ambao utakuwa na tija kwa wafanyabiashara.


"Tuache kudanganyana mimi nimefika Dubai nimejionea namna bandari za wenzetu zinavyofanya kazi, uwekezaji unaofanywa na Rais utasaidia sisi wafanyabiashara malalamiko ya kucheleweshewa mizigo bandarini yatakwenda kuisha, Mimi sikubaliani kwamba wabunge wa Ccm Hatuma akili tukinyamaza tunaonekana vilaza".amesema Musukuma


Na Kuongeza "sakata linaloendelea kwenye mitandao ya kijamii na mimi nimetajwa Sioni ajabu wala siogopi kusema mimi ni mmoja wa wabunge ambao tulisafiri kwenda kujifunza na kuona uwekezaji nchini ikiwa ni kawaida ya Bunge huwa kuna bajeti ya

wabunge kusafiri kwenda nchi mbalimbali

kujifunza, sasa kwa imani iliyopo ni kwamba wabunge wote walioenda Dubai wamehongwa kwa ajili ya kutetea bandari".Ameongezea Musukuma


Amesema Moja ya changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni pamoja na kuchelewa kwa mizigo bandarini hivyo uwekezaji huo utasaidia kupungua kwa urasimu wa kuchelewa kwa mizigo.


"Nitashangaa sana kwa mfanyabiashara yeyote anayepitisha mizigo katika bandari ya Dar es Salaam ukiacha hawa wapiga kelele, akipinga jambo kubwa hili la kihistoria linalotarajiwa kufanywa na serikali ya awamu ya sita". Amesema 


Aidha amesema ataendelea kupambana na wanaoendelea kuiponda serikali na kusambaza uzushi kwenye mitandao ya kijamii na kuamua kutengeza uongo na kuzua taharuki kwa watanzania na wengine kudai amehongwa ili kutumika kwenye sakata hili la bandari."Naomba niwaonye wale wote wanaoendelea kusambaza maneno kwenye mitandao ya kijamiii wanaosema nimehongwa ili kutetea hili suala niwaambie tu mimi nimeanza kumiliki magari na vitu vya thamani kabla hata sijawa mbunge na serikali inapoleta jambo zuri siwezi kupingana nalo haswa ukizingatia suala la bandari nilienda mwenyewe dubai nikashuhudia hivyo wasinichokoze kwani nina mengi sana yakuzungumza lakini nimeamua kukaa kimya lakini wakitaka nizungumze nitazungumza tu maana sina cha kuogopa na kwenye ukweli lazima tuseme ukweli hii nchi ina wasome wengi ambao wamekaririshwa badala yake wanashindwa kuchanganua mambo hivyo ningewaomba wasomi wanchi kutumia elimu zao vizuri na sio kupotosha watanzania".Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: