Katibu wa CCM Nachingwea Mwanaisha Ame Mohamed akitoa taarifa Kwa kamati ya siasa mkoa wa Lindi walipofanya ziara wilaya ya Nachingwea
Katibu wa CCM Nachingwea Mwanaisha Ame Mohamed akitoa taarifa Kwa kamati ya siasa mkoa wa Lindi walipofanya ziara wilaya ya Nachingwea
Na Fredy Mgunda, Nachingwea.CHAMA Cha mapinduzi wilaya ya Nachingwea (CCM) kimewataka madiwani wote wa chama hicho kufanya mikutano ya hadhara ili kutatua kero za wananchi.

Akitoa taarifa ya kwa kamati ya siasa mkoa wa Lindi,katibu wa CCM Nachingwea Mwanaisha Ame Mohamed alisema kuwa madiwani wengi hawataki kufanya mikutano ya hadhara katika kata zao na kusababisha chama kutumia nguvu kubwa kutoa elimu Kwa wananchi.

Mohamed aliimbia kamati ya siasa mkoa wa Lindi kuwa wananchi wengi wanakero nyingi ambazo wanatakiwa kutatuliwa na madiwani wa kata husika.

Alisema kuwa mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amekuwa akifanya kazi kubwa kusikiliza na kutatua kero za wananchi na kukijenga chama 

Aidha katibu Mohamed alisema kuwa wameshafanya chaguzi kwenye maeneo yote ambayo yalikuwa hayana viongozi wa kichama.

Alimazia kwa kuiomba kamati ya siasa mkoa wa Lindi kutoa kadi za chama Kwa wakati ili wananchi na Wanachama waweze kupata haki ya kukitumikia chama.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: