Katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Mafinga Ndugu, Ayoub Kambi akisikiliza changamoto za watumishi kata ya Bumilayinga
Hakikisheni mnaweka wazi  na kuwasomea wananchi mapokezi ya fedha zote mnazopokea za miradi ya maendeleo  kwenye mikutano ya Kata na mbao za matangazo kwani wananchi wanahaki ya kujua mapato na matumizi ili kujua nini serikali inafanya na kufahamu Miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Kata husika.

Akizungumza kwenye ziara ya Mkurugenzi ya Kusikiliza changamoto za watumishi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu, Ayoub Kambi amesema kuwa Katika Utumishi kuna Haki na Wajibu, hivyo kila mtumishi ahakikishe anatimiza wajibu wake anapodai Haki.

“ Nimepokea changamoto zenu na nitazufanyia kazi na ndo mana nimekuja na wataalamu wangu ili lile linaloweza kutatulika liishe na Yale yanayohitaji ufuatiliaji nayachukua kwa Utekelezaji “

Amesema malalamiko ya wananchi ngazi ya kata yatatuliwe na wananchi Wasikilizwe kwa kutumia lugha mzuri. Aidha ameagiza Wataalamu Makao Makuu kufanya ziara na kutoa ufafanuzi kuhusu Masuala ya haki za watumishi na sera mbalimbali ili kuwajengea uelewa watumishi ngazi ya Kata.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Watumishi wote Kata ya Bumilayinga na Baadae Kata ya Isalavanu wakiongozwa na Kaimu Mtendaji wa Kata ya Bumilayinga ndugu,Nikanileka Chaula, Mtendaji Kata ya Isalavanu Calvina Msovela, Wataalamu kutoka Makao Makuu Idara ya Utawala, Elimu Msingi na Sekondari .

Ziara ya Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Ayoub Kambi Ni ziara ya kimkakati ambayo imeanza tarehe 21/6/2023 mpaka tarehe 6/7/2023.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-MAFINGA TC

Sima Bingileki 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini -Mafinga TC
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: