Mkuu wa Wilaya  ya Arumeru  Mhe.Emmanuela Kaganda aelekeza miradi ya uboreshaji miundombinu katika shule za Msingi   kukamilika kwa Wakati na kwa ubora uliokusudiwa.

Mhe.Kaganda  amesema  hayo  wakati  wa  ziara ya kukagua utekelezaji wa  Miradi  ya  BOOST  katika Halmashauri ya  Wilaya  ya  Meru ambapo  Serikali imetoa milioni  961.5  za  uboreshaji  miundombinu ya elimu kwenye Shule  za Msingi.

Aidha, Mhe. Kaganda  amesema Serikali  ya  Dkt.Samia  Suluhu  Hassan  imejipanga vyema kuendelea kuwaletea  wananchi wake maendeleo ambapo imetoa  fedha nyingi za maendeleo katika sekta ya elimu,afya, maji nk

Mhe.Kaganda  amewataka   wataalum wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimamia vyema utekelezaji wa miradi hiyo  kukamilika kwa wakati na kuwa na ubora uliokusudiwa kwani anmza ya Serikali ni kuwawezesha Watoto wa kitanzania kupata Elimu bora katika mazingira rafiki.

Share To:

Post A Comment: