WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ametii maagizo ya Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo ya kumtaka kushughulikia tatizo la maji Kata ya Uhambingeto wilayani Kilolo mkoani Iringa huku akitoa ahadi ya mradi huo kukamilika ifikapo Oktoba mwaka huu.


Aidha Waziri Aweso amewaomba radhi wananchi wa kata hiyo pamoja na viongozi wa wilaya na mkoa kutokana na kukwama kwa mradi huo ambao tayari fedha zake zilishatolewa na Rais Samia Suluhu Hassan huku akikiri hadharani mradi huo umechelewa kutokana na uzembe na wala hakuna sababu nyingine yoyote.

Siku za hivi karibu Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo alipokea malalamiko ya wananchi kuhusu kukwama kwa mradi huo na hivyo kusababisha changamoto ya uhaba wa maji, hivyo alitoa maagizo kwa Waziri wa Maji na watalaam wake kufika kwenye kata hiyo na kutafuta ufumbuzi.

Akizungumza leo Mei 2, 2023 , Waziri wa Maji Jumaa Aweso mbali ya kuwaomba radhi wananchi amesema Rais Dk.Samia Suluhu Hassan wakati anahutubia Bunge alisema yeye ni mama na hayuko tayari kuona akina mama wanateseka kwa adha ya maji.

“Akanipa maelekezo mahususi kuhusu Wizara yetu akisema kwamba yeye ni mama na anasilimia kubwa ya watanzania wanaoteseka juu ya adha ya maji ni akina mama.Rais alisema kuona wamama wa nchi hii wanahangaika na adha ya maji.Akaniambia nikizingua atanizingua.

“Sasa ambacho nataka kusema mbele yenu wazazi wangu Wizara ya Maji jukumu letu watu wapate maji, kwa hiyo hapa hata niseme vipi wananchi wanachotaka maji, hawataki maneno.Rais wetu ameshatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi huu,”amesema Waziri Awesu.

Ametumia nafasi hiyo kufafanua amepata maelezo ya kutosha kuhusu mradi huo , ulazaji wa mabomba ulikuwa kilometa 35 lakini kazi ambazo zimefanywa ulazaji wa mabomba ni kilometa 31 umeshafanyika na zimebaki kilometa nne.

“Kazi ilikuwa ya ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa maji lita 100,000 kwa ajili ya kuhifadhi maji, ujenzi wa vituo vya maji 14 ambavyo ujenzi wake haujakamilika. Kwa hiyo kwenye ujenzi wa miradi ya maji kazi kubwa inakuaga kwenye ulazaji wa mabomba a hapa kazi imefanyika kunbwa.Baada ya kuangalia mradi huu ujenzi umefanyika kwa asilimia 55 bado 45

“Hata hivyo tulivyokuwa na lengo la kujenga mradi huu wananchi mlifurahi kwasababu mnaenda kuondokana na adha ya maji, tunafahamu mtu anapokosa maji, adha inakuwa kubwa na ndio maana nimewaomba radhi.Niwahakikishie mradi huu utakamilika ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa na hatutakuwa na Mswalie Mtume.”

Amesema Wizara ya Maji ni wauza duka na wenye duka ni Chama Cha Mapinduzi(CCM) sipo tayari kuona leo tunazungumza na wananchi halafu Katibu Mkuu wa CCM alishatoa maelekezo.Wizara ya Maji hawana kisingizio kuhusu utekelezaji wa mradi huo kwani fedha zipo.

“Kusema ukweli hakuna kisingizio ila uzembe ndio umetokea kwenye mradi huu, kwa hiyo maelekezo yaliyotolewa ndani ya miezi mitatu watu wanywe maji , nitasimamia haya na lazima mnywe maji.Watu hawataki maneno mengine wanataka maji,”amesema.

Ameongeza kuwa yeyote atakayezingua kuhusu mradi huo akamatwe awekwe kituoni kwani hayuko tayari kuona wananchi wanakosa maji wakati fedha iko, hilo haliwezekani.

“Kuanzia kesho tunataka kuona kazi ya ujenzi wa vituo vya maji unaanza , diwani utatupa taarifa, kama wangekuwa hawana fedha tungesema shida ni fedha lakini zipo .Hata hivyo niwaambie mwisho wa ziki sio ziki bali baada ya ziki ni faraja,nataka niwatie moyo faraja yetu ni Dk.Samia Suluhu Hassan.

“Kazi ambayo anaifanya katika taifa letu sio mchezo, ameingia kipindi kifupi lakini kazi anayofanya ni kubwa mno, leo mradi huu ni zaidi ya shilingi bilioni moja na Rais ametoa zote, tusikwamishe jitihada za rais, na tukiona mtu anataka kukwamisha hata kama ana mapembe marefu kiasi gani tuyakate.”WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akizungumza mbele ya Wananchi leo Juni 2,2023 katika Kata ya Uhambingeto wilayani Kilolo mkoani Iringa kushughulikia tatizo la mradi wa maji ambao umekwama kwa mda mrefu wakati tayari fedha zake zilishatolewa na Rais Samia Suluhu Hassa.

















Mbunge Viti Maalum mkoa wa Iringa (CCM) Mh. Ritta Kabati akifurahia jambo mara baada ya Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso kutolea majibu ya kukwama kwa mradi wa maji katika Kata ya Uhambingeto wilayani Kilolo mkoani Iringa
Mbunge wa jimbo la Kilolo Mhe.Justine Nyamoga akishukuru kwa ujio wa Waziri wa Maji Mhe.Juma Awezo kuja kutatua changamoto ya mradi wa maji katika Kata ya Uhambingeto wilayani Kilolo mkoani Iringa

Share To:

Post A Comment: