Mikoa ya Arusha na Mtwara imeanza vizuri katika michezo ya Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023) iliyochezwa Juni 16, 2023 Mjini Tabora.

Mabingwa watetezi wa Mpira wa Kikapu wasichana Mkoa wa Arusha, walikutana na Mkoa wa Katavi katika Mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Tabora Wavulana Majira ya saa 10 Jioni, Arusha wakiibuka na Ushindi wa magoli 37 -6.

Katika mchezo mwingine wa Kikapu Wasichana, Mkoa wa Mwanza uliibuka na ushindi wa magoli 42 -28 dhidi ya Manyara, na Singida ikaifunga Shinyanga 25 -11, huku Kilimanjaro ikiadhibu Katavi 20 -10.

Mchezo mwingine uliwakutanisha Songwe na wenyeji Tabora, ukimalizika kwa Tabora kupata ushindi wa 9-4, huku mchezo pekee wa wavulana uliochezwa jioni ukimalizika kwa Dar es salaam 49 Geita 5.  

Upande wa Soka Wavulana kwenye uwanja  A wa shule ya Sekondari Tabora Wavulana ulichezwa mchezo mkali na wa kusisimua kati ya Mtwara na Morogoro, ambao ulimalizika kwa Mtwara kuibuka na ushindi wa 3-1.

Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023) ambayo yalifunguliwa Tarehe 15 Juni 2023, yanaendelea katika viwanja mbalimbali vya shule za sekondari Wasichana na Wavulana Tabora.

Share To:

Post A Comment: