Waandishi wa habari wakifatilia hotuba ya Waziri wa Habari,Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Nape Nnauye (hayupo pichani) wakati , akizungumza na waandishi hao mara baada ya kukutana na Kamati ya kufanya tathimini ya hali ya uchumi wa vyombo vya habari nchini.

Mwenyekiti wa Kamati  ya Kutathmini Hali ya Uchumi ya Vyombo vya Habari na wanahabari Bw.Tido Muhando,akizungumza mara baada ya Waziri wa Habari,Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Nape Nnauye (hayupo pichani)  kukutana na Kamati hiyo.

Na Gideon Gregory, Dodoma.

Waziri wa Habari,Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Nape Nnauye, ametoa wito Kwa Wamiliki wa Vyombo vya Habari,Wanahabari na Wadau wa Habari kutoa ushirikiano Kwa Kamati Kutathmini Hali ya Uchumi ya Vyombo vya Habari na wanahabari ili kuisaidia kukamilisha kazi yake Kwa ufanisi.

Waziri Nape ameyasema hayo leo Mei 23,2023,Jijini Dodoma,wakati  akizungumza na waandishi mara baada ya kukutana na Kamati ya kufanya tathimini ya hali ya uchumi wa vyombo vya habari nchini.

Waziri Nape amesema kuwa kazi ya Kamati hiyo ni kubwa hivyo inahitaji umakini katika utekelezaji wake kwani ndio imebeba hatma ya Vyombo vya Habari na Waandishi wa habari.

Amesema ana matumaini kuwa Kamati hiyo itatumia vyema Miezi sita iliyopewa kufanya tathmini na kuja na ripoti kamili itakayokuwa imebeba maslahi ya Vyombo vya Habari na wanatasnia na Dkt.Samia anasubiria ripoti hiyo hivyo wakae wakijua kuwa taifa zima lipo kimya kusubiria watakuja na kipi.

“Nimekutaka na Kamati hii awali tulikuwa tumeipa miezi mitatu lakini kutokana na umuhimu wa tasnia hii na maagizo ya Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa jambo hili lisifanywe kwa kuharakishwa bali lifanywe kwa umakini wa hali ya juu ili kuleta mabadiliko katika tasnia hii”amesema Waziri Nape

“Nitoe wito Kwa Wanahabari na Wadau wa habari kuiunga mkono hii Kamati penye kuhitaji kushauri washaurini kama Kuna kosa sehemu waambieni ili kuja na ripoti iliyokamilika Kwa maslahi ya Tasnia ya habari nchini.

Pia Mhe.Nape amesema kupitia Wizara yake itasimamia madeni yote yanayodaiwa na Vyombo vya Habari Serikalini na kwenye Taasisi zinalipwa hata kama sio Kwa pamoja ila waanze kulipwa kidogokidogo iwezekanavyo.

“Tunapozungumzia Ustawi wa Vyombo vya Habari nchini huwezi kuacha kugusia Madeni yaliyopo Serikali na kwenye Taasisi kwani Fedha hizo ndio zinazotakiwa kutatua changamoto zinazoikabili hivyo nitahakikisha pesa hizo zinalipwa hata kidogokidogo,”Amesema Mhe.Nape

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw.Tido Mhando amesema kuwa watafanya kazi hiyo Kwa umakini bila kukurupuka kwani Serikali inasubiri taarifa kamili ili kuepukana na kutoa taarifa ambayo haijajitosheleza.

“Tumekaa tukatathimini na kubaini kwamba Muda tulikuwa tumepewa ni mdogo sana ukilinganisha na uzito wa jambo lenyewe ambalo linatakiwa kuja na majibu yaliyojitosheleza kwani sisi tumebeba Maslahi ya Tasnia ya Habari,

Aidha ameongeza na kuwa wameomba kuongezewa Muda mpaka Mwezi Novemba 2023 na kuishukuru Serikali kupitia Wizara ya Habari kwa kuridhia ombi hilo baada ya kuona ukubwa wa kazi hiyo.

Awali Kamati hiyo ilipewa Muda wa Miezi mitatu kukamilisha ripoti yake ila baada ya kuwashirikisha wataalamu kutoka Vyuo Vikuu na TCRA na kupata tathmini ya kitaalamu ndipo wakabaini kuwa kazi hiyo ni kubwa tafouti na walivyokuwa wanafikiria wameomba kuongezewa miezi mingine sita.

Share To:

Post A Comment: