Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Shirika lisilo la kiserikali la Nancy Foundation limetembelea shule ya msingi Kitangili iliyopo Manispaa ya Shinyanga na kutoa msaada kwa watoto waliokuwa wakiishi na kufanya kazi mtaani ambao kwa sasa wanaeendelea na masomo yako shuleni hapo.

Limetoa msaada kwa watoto hao ikiwa ni sehemu ya kutekeleza mradi wa kupunguza au kumaliza tatizo la watoto wanaoishi mitaani na kwamba shirika hilo la Nancy Foundation linashirikiana na serikali katika hatua mbalimbali za kuimarisha usalama wa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa shirika la Nancy Foundation  Bwana Ezra Manjerenga amesema wametoa msaada wa chakula na kusaidia kuwalipia gharama za masomo ya ziada wanafunzi waliokuwa wakiishi mtaani.

“Leo tumefika shule ya msingi Kitangili kilichotuleta hapa ni kuendeleza ufuatiliaji wa wale watoto waliokuwa wakiishi na kufanya kazi mitaani hapa shuleni tumebaini watoto saba mahitaji yao muhimu waliyoyaomba ikiwemo vifaa vya shule lakini tunachokiangalia ni kupunguza muda wao wa kukaa mtaani”

“Leo tumewalipia watoto wote hawa gharama zao za chakula shuleni lakini pia tumewalipia hela ya muda wao wa ziada (Tuition) pamoja na bima ya afya CHF ambayo tayari wazazi wao tuliwasaidia na kikubwa katika mradi wetu tunataka moyo wao warudishe nyumbani na tupunguze changamoto ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani”amesema Ezra

Aidha Mkurugenzi wa shirika la Nancy Foundation Bwana Ezra Manjerenga ameikumbusha serikali kuendelea kushirikiana katika hatua mbalimbali za kuwaendeleza watoto hao.

“Tunawataka maafisa ustawi wa jamii, maafisa maendeleo ya jamii na polisi dawati la jinsia na watoto kuhakikisha kwamba wanaendeleza, tayari wanatakwimu za idadi ya watoto wanaozurula, tayari watoto wanaelimu ya maadili na tayari watoto wapo shuleni sasa tunataka tuone mikakati ya serikali kuendelea kufuatilia mienendo ya watoto ili kutengeneza watoto ambao ni washindi kwa kutengeneza historia yao ya kuwatoa mitaani “.

“Mpaka sasa tuliofanikiwa kuwarudisha kwenye familia zao wapo watoto 22 na lengo letu lilikuwa tufikie watoto 30 lakini watoto ambao tuliwakuta mitaani na wamefanyiwa dodoso kuhusu maisha yao tunajumla ya watoto 38 ambapo wengine tunaona wanachangamoto za kawaidi tu sisi tunachukua tunaobaini kweli wanachangamoto kubwa hasa zinazokwamisha masomo yao shuleni” amesema Bwana Ezra

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule ya msingi Kitangili Mwalimu Rachel Dembe amelishukuru shirika la Nancy Foundation kwa kutoa msaada huo na kwamba itasaidia kupunguza changamoto za watoto hao.

“Kwa niaba ya uongozi wa shule sisi tunawashukuru sana Nancy Foundation kwa jinsi ambavyo mmetusaidia kuwahudumia hawa watoto ili waweze kuhudhuria masomo yao bila kukosa  kwa sababu muda mwingine tulikuwa tunapata wakati mgumu kuwatafuta lakini tunashukuru kwa msaada mliotupa wa chakula pamoja na kuwalipia hela ya masomo ya ziada tunategemea hili litakuwa chachu kwa wanafunzi hawa kuhudhuria shuleni na sisi tunaahidi tutajitahidi kuwasimamia kama ipasanyo”.amesema Mwalimu Rachal

Naye Mtendaji wa kata ya Kitangili Mayala Ibrahim amelishukuru shirika hilo la Nancy Foundation kwa kutoa msaada huku akiahidi kuendelea kushirikiana ili kutimiza mpango wa srikali juu ya elimu bora kwa watoto.

Mashirika mawili yasiyokuwa ya kiserikali Mkoani Shinyanga Nancy Foundation na Ubongo learing yanatekeleza mradi wa kupunguza au kumaliza tatizo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani, mradi huo unaoitwa “Home is where the heart is”.Mkurugenzi wa shirika la Nancy Foundation Bwana Ezra Manjerenga na afisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Lemiflora  Nyalanja upande wa kulia, wakiwa kwenye ofisi ya mwalimu mkuu shule ya msingi Kitangili.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: