Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila akisimamia utiaji saini ujenzi wa bara bara ya Labay-Haydom kwa kiwango cha lami km 25 chini ya kampuni ya Jiangxi Geo Engineering Group.
Naibu waziri wa Ujenzi na uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya akizungumza mara baada ya kushuhudia tukio kubwa la kusainiwa kwa mikata ya ujenzi wa bara bara Labay-Haydom kilimita 25.





Na John Walter- Manyara

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,  Mhandisi Godfrey Kasekenya ameshuhudia utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Barabara ya Labay-Hydom  (KM 25) kwa kiwango cha Lami uliosainiwa Leo Wilayani Mbulu Mkoani Manyara.

 

Gharama ya mradi huo ni kiasi cha shillingi billion 42,271,419,932.88  ambayo itajengwa na Kampuni ya Jiangxi Geo Engineering Group Limited  kwa muda wa miezi 18.

 

Hafla ya utiaji Saini mkataba wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Labay-Haydom km 25 imefanyika Viwanja vya Mahakama ya Haydom Mbulu leo Mei 19,2023 na kushuhudiwa na mamia ya wananchi.

 

Mtendaji mkuu wa TANROADS Tanzania Mhandisi Rogatus Mativila amesema  Kukamilika kwa bara bara hiyo kutachochea Shughuli za Maendeleo katika mkoa wa Manyara.

 

Kwa mujibu wa Mtivila, barabara ya Serengeti Southern Bypass Karatu-Mbulu-Haydom-Sibiti-Lalago hadi Maswa kilomita 389 inaunganisha mikoa ya Arusha,Manyara,Singida na Simiyu ambapo Mkoa wa Manyara una jumla ya Kilomita 113 ikijumuisha Kipande cha Labay-Haydom.

 

Mhandisi Godfrey Kasekenya amemtaka mkandarasi Kufanya kazi Kwa weledi na kumaliza kwa muda uliopangwa na gharama husika.

 

Amesema mradi huo ni mpango wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Suluhu Hassan kuwawekea Wananchi Mazingira Bora ya kufanya Shughuli zao za Maendeleo.

 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere licha ya kumshukuru Rais Samia Suluhu kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi huo, amemuomba Rais kuendelea kutoa fedha zaidi ili kuongeza zaidi mtandao wa bara bara za  lami Mkoani humo. 

 

Naye Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Flatery Massay ameishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa za kujenga bara bara hizo kwa kiwango cha lami zinazounganisha mikoa ya Manyara,Singida na Arusha.

 

Aidha ameiomba serikali kujenga bara bara za lami kutoka Haydom Katesh,Mbulu-Dareda.

 

 

 

Share To:

Post A Comment: