John Walter- Kiteto

Mradi huu ufikapo June 30.2023 utakuwa umekamilika kwa kufungua mawasiliano ya wananchi wa kata za Ndedo na Makame Kiteto ambayo hayakuwepo.

Meneja wa Tarura Kiteto, mhandisi Edwine Magiri Leo  Leo Mei 14.2023 ametaja urefu wa  barabara hiyo kuwa ni km 26.8 ambazo zinatengenezwa kwa fedha za Serikali.

"Fedha hii ni zao la tozo ya sh 100 kwa lita ya mafuta ambayo inatozwa na Serikali"alisema mhandisi Magiri

"Kutoka Ndedo hadi Makame ni kata mbili tofauti ambapo kata hizi zilikuwa hazija unganishwa na barabara kwa hiyo barabara hii tunaifungua ili wananchi hawa waweze kupata huduma muhimu za jamii ambazo awali hazikupatikana kwenda kwa urahisi maeneo ya Kibaya na barabara kubwa inayoanzia Ndedo hadi Arusha"

Amesema mradi huu una gharimu sh 514mil ambapo inategemewa ifikapo June 30.2023 mradi utakuwa umekamilika na kuanza kutumika

"Tunaye hapa mkandarasi kama unavyomuona ameanza kazi na mashine zake zote ziko saiti, hadi itakapofika mwezi wa sita mwaka huu mradi utakuwa umekamilika na kuanza kunufaisha wananchi wa kata hizi mbili Ndedo na Makame ambazo hazikuwa na mawasiliano ya barabara muda mrefu"alisema mhandisi Magiri.

"Ninachoweza sema hapa mradi huu utakapo tekelezwa na kukamilika, wananchi wa maeneo haya sasa  watunze miundombinu ya barabara hii kwa sababu awali hawakuwa na barabara kwa zaidi ya miaka 60 ya Uhuru hivyo barabara hii itaongeza vipato vyao kama unavyoona hapa tuko kwenye mbuga kuna uhifadhi unaoendelea kwa hiyo ni kiungo muhimu sana kwa wananchi wa maeneo haya"

Amesema mara nyingi wananchi walilazimika kutumia usafiri wa pikipiki hivyo huduma ya afya na elimu kwa maeneo haya ilikuwa changamoto

Ally Mgoya Mwananchi kata ya Ndedo alishukuru Serikali kwa kuona haja ya kujenga miundombinu hiyo ya barabara akisema usafiri wa pikipiki uliwalazimu kutumia sh 30 elfu kwenda na kurudi na kujikuta wakitumia fedha nyingi kuliko kufanya maendeleo mengine

"Hili eneo ni mbuga  wakati wa masika halipitiki usafiri pekee ni pikipiki ukitaka kwenda kata ya Makame kutoka Ndedo lazima utumie sh 30 elfu za kwenda na kurudi ambapo ni km 26.8" alisema Mngoya

Share To:

Post A Comment: