MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango kesho anatarajiwa kuanza ziara ya siku nne mkoani Arusha, ikiwemo kuweka jiwe la msingi kwenye makao mapya ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA).

Ziara hiyo ya siku nne itaanza kesho kwa kusalimia wananchi eneo la Mto wa Mbu, kisha ataenda wilayani Karatu na kuweka jiwe la msingi kwenye makao makuu mapya ya NCAA.

Akizungumza na wanahabari, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema katika juhudi za kuimarisha uhifadhi, NCAA ilihamisha ofisi zake kutoka ndani ya mamlaka hiyo na kupeleka nje, ili kulinda uhifadhi.

Amesema pia ataenda kuweka jiwe la msingi Hospitali ya Wilaya ya Karatu iliyogharimu kiasi cha Sh bilioni 3 na kusema kuwa hospitali hiyo ni ya kiwango cha juu.

Mongella amesema Mei17 ataelekea Wilayani Ngorongoro na kusalimia wananchi eneo la Wasso na Sale kwa ajili ya ufunguzi wa barabara kutoka Loliondo -Wasso-Sale.

“Nawaomba wananchi wajitokeze kumlaki Makamu wa Rais na pia tuunge mkono juhudi zinazofanyika katika nchi yetu hususan katika maendeleo, ” amesema.

Share To:

Post A Comment: