MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameendelea na ziara yake jimboni ambapo Mei 6,2023,ametembelea Kata ya Issuna katika Kijiji cha Issuna A kilichopo wilayani Ikungi Mkoani Singida.

Akiwa katika ziara hiyo amezungumza na wananchi wa kijiji hicho kupitia mkutano wa hadhara na kusikiliza kero zinazowakabili.

Akizungumza katika mkutano huo ,Mh Mtaturu
amewakumbusha juu la suala la miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika Kata hiyo ya Issuna.

“Ndugu zanguni sote tunaona kazi nzuri anayoifanya mama yetu,Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan katika jimbo letu,tunaona fedha zinavyokuja na miradi inatekelezwa kwa kasi,sote sisi kwa imani zetu tumuombee Mungu amlinde na amsimamie katika majukumu yake,”amesema.

Wananchi wa kijiji hicho cha Issuna A wamempongeza Mh Mtaturu kwa uchapakazi wake na kumuahidi kumpa ushirikiano kwa lengo la kukijenga kijiji chao kwa maendeleo zaidi.

“Tunasema asante sana Mh. Mtaturu na hakika kazi yako iliyotukuka katika Jimbo la Singida Mashariki inaonekana na,wewe ni mtumishi wetu na kiukweli unatutumikia ipasavyo,pokea shukrani zetu za dhati kabisa,”.

     Facebook


Share To:

Post A Comment: