Na John Walter-Babati

Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Manyara imempongeza Mbunge wa Babati Vijijini kwa kufanya ziara mara kwa mara jimboni mwake kuzungumza na Wananchi na kutatua kero zao.

Pongezi hizo zimetolewa leo Mei 7,2023 na  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Manyara Joanes Darabe wakati akizungumza na Wazazi,Wanafunzi na wakufunzi katika chuo Cha Ualimu Mamire ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya wiki ya Wazazi inayofanyika kitaifa mkoani Manyara.

Amesema katika Shule mbalimbali za Msingi na Sekondari,Mbunge huyo ametoa mashine za kuchapisha mitihani na Komputa na misaada mingine kuboresha elimu.

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Taifa Mheshimiwa Dogo Iddy Mabrouk amesema Mbunge Sillo anatosha na kwamba Chama kinahitaji Viongozi wa aina hiyo wanaojituma kwa ajili ya wananchi.

Wiki ya Wazazi mwaka 2023 Kilele chake kitaifa kitafanyika mjini Babati mkoani Manyara Mei 9,2023 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa Mheshimiwa.

Kauli mbiu ya wiki ya Wazazi mwaka huu Taifa Bora hutokana na malezi Bora ya watoto.

Share To:

Post A Comment: