Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde leo amegawa vifaa vya michezo kwa Timu ya UMITASHUMTA Dodoma Jijini inayoshiriki mashindano ya michezo ya Shule za Msingi Mkoani Dodoma.


Mbunge Mavunde amegawa vifaa hivyo vyenye thamani ya Tsh 3,000,000 leo wakati akizungumza na wanafunzi hao ambao wameweka kambi ya mafunzo katika Shule ya Sekondari Dodoma na kuwataka kuwahakikisha wanafanya vizuri katika mashindano hayo ambayo yanashirikisha na Timu zingine za wilaya za mkoa wa Dodoma.

Katika kuunga mkono juhudi za kuimarisha michezo Jijini Dodoma,Benki ya Watu wa Zanzibar(PBZ),Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) na Kampuni ya Nicas Alminium ni miongoni mwa Kampuni zilizochangia vifaa vingine vya michezo.

Akishukuru kwa niaba,Afisa Elimu Msingi Jiji Mwl. Prisca Myalla amemshukuru Mbunge Mavunde na wadau wote wa michezo kwa kuwatia moyo wanafunzi hao na kuahidi kusimamia ipasavyo timu hiyo ya wanafunzi ili iweze kufanya vizuri katika mashindano hayo ya mkoa  na kuliletea sifa Jiji la Dodoma. 

Share To:

Post A Comment: