Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ameendelea kutelekeza ahadi yake kwa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya kuchangia mradi wa ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT na vyumba vya biashara.

Awali Mahundi ambaye pia ni mjumbe wa Baraza Kuu la UWT Mkoa wa Mbeya aliahidi kuchangia shilingi 20m ambapo alitanguliza shilingi 5m na sasa amechangia shilingi 5m hivyo kufanya jumla fedha alizotoa kuwa ni shilingi milioni kumi.

"Kiu yangu ni kuona wanawake wanapiga hatua kiuchumi hivyo kutimiza ndoto yangu ya tukue pamoja"alisema Mahundi.

Katika ziara yake ya kujitambulisha mwaka jana Mahundi alizitembelea Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya na kuwakabidhi fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo.Share To:

Post A Comment: