Na; Elizabeth Paulo, Dodoma

Jeshi la Polisi Tanzania limetoa onyo Kali kwa wahalifu wasiotaka kuachana na vitendo vya kihalifu na kufanya kazi halali nakwamba Sheria Ina mkono Mrefu hivyo watakamatwa wakati wowote.

Kauli hiyo Imetolewa leo Mei, 12, 2023 jijini Dodoma na Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP -David Misime mbele ya waandishi wa Habari alipokua akieleza Mafanikio wanayoyapata kama Jeshi la Polisi katika kubaini, Kuzuia, na Kutanzua uhalifu kwa ushirikiano kutoka kwa wananchi.

"Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa wahalifu ambao hawataki kuachana na vitendo vya kihalifu ili kufanya kazi halali, Watambue kuwa wakifanya uhalifu wowote ule iwe Mchana au Usiku ni lazima watakamatwa kwa njia yeyote na itakua ni aibu kwao na familia zao."Amesema SACP Misime

Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Jeshi la Polisi SACP- Misime Ametolea ufafanuzi wa kukamatwa kwa watuhumiwa waliohusika na mauwaji yaliyotokea hivi karibuni yaliyomhusu Daktari Isack Daniel nakwamba Watuhumiwa watatu waliofanya mauaji hayo pamoja na kukimbilia Mwanza na baadaye Dar es Salaam wamekamatwa na askari waliobobea katika uchunguzi wa matukio ya mauaji.

"Mtakumbuka mei 3, 2023 yaliripotiwa mauaji ya DK. Isack Daniel Athumani ambaye alikua Mganga Mfawidhi wa kituo Cha Afya Kerende kilipocho Tarime Rorya Akitokea kazini, Tukio hilo lilifanywa na watu ambao hawakuweza kufahamika kwa mara Moja, sasa hao watatu tumewakamata na Uchunguzi unakamilishwa ili waweze kufikishwa mahakamani". Amesema

Pia amesema kutokana na Uchunguzi makini wa askari wanaochunguza matukio ya mauaji wamefanikiwa kukamata watuhumiwa watatu kuhusiana na mauaji ya mfanyakazi mmoja wa Mgodi wa GGM  Milembe Selemani aliyekua maarufu kwa jina la Hungwa siku ya Aprili 26, 2023 katika mtaa wa Matulole kata ya Buhalahala Mkoani Geita.

SACP- Misime Amesema watuhumiwa hao  wameonyesha vielelezo walivyotumia katika Mauaji hayo ikiwa ni pamoja na baadhi ya mali za marehemu, na watafikishwa mahakani wakati wowote.

"Mtuhumiwa wa nne katika tukio hili baada ya kupata taarifa ya kukamatwa kwa wahalifu wenzake na kwamba askari wamefika nyumbani kwake, aliamua kujihukumu  mwenyewe kwa kujinyonga, Mtuhumiwa huyo amejulikana kwa majina ya Pastory Lugodisha @ Buchuchu na alijinyonga mei 06, 2023 kwa kutumia mkanda wa suruali katika pori la hifadhi ya Buhindi Wilayani Sengerema".Ameeleza SACP- Misime 


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: