NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),  Deogratius Ndejembi amesema serikali itapeleka shilingi milioni 800 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Masieda na ununuzi wa Vifaa Tiba kwa ajili ya kituo hicho.

Ameeleza hayo wakati alijibu Swali la Flatei  Massay, Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, aliyetaka kujua Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kumalizia ujenzi wa Vituo vya Afya Geterer na Masieda.

Ndejembi amesema katika mwaka wa fedha wa 2023/24, Halmashauri Mbulu, imetengewa Shilingi milioni 200 kwa ajili ya ukamilishaji wa Kituo cha Afya Marekadu.
Aidha, Amesema Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi, ukamilishaji na ukarabati wa Vituo vya Afya ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa Kituo cha Afya Geterer kwa kadri fedha inavyopatikana.

Ndejembi amesema Serikali inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na umaliziaji wa maboma ya Vituo vya afya kote nchini.
Share To:

Post A Comment: