Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi kupitia chama cha mapinduzi CCM, Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko amewaasa viongozi na wanachama  kuendelea   kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo ili kuimarisha jumuiya hiyo.

Ametoa kauli hiyo leo Mei 11,2023 katika ziara yake ya kamati ya utekelezaji ya umoja wa wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini iliyolenga kutembelea na kukagua uhai wa chama kwenye kata ya Ibadakuli pamoja na kata ya Kolandolo ambapo Mwenyekiti huyo amesisitiza umoja ili kuijenga jumuiya na kuleta maendeleo katika jamii.

Bwana Mrindoko amewaomba viongozi na wanachama kuanzisha miradi itakayowanufaisha wao na jumuiya kwa ujumla huku akisisitiza umoja na kuepuka migogoro ili kufikia mipango iliyokusudiwa na jumuiya hiyo.

Amesema ni muhimu viongozi wa jumuiya hiyo kata kusimama imara katika usimamizi wa ilani ya CCM na kwamba wasikatishwe tamaa na watu wenye nia mbaya na maendeleo yanayoletwa na viongozi wa serikali kwenye  jamii na Taifa kwa ujumla.

“Tusiwe jumuiya ya kudharaulika tunataka iwe jumuiya ya maendeleo niwaomba wana jumuiya ya wazazi msikate tamaa kwahiyo tushirikiane katika shughuli hizi za maendeleo lakini niwaomba tubuni miradi kuanzia kwenye matawi na kata tuwe na miradi ya kujisimamia sisi wenyewe tusimame imara katika hili”.

“Niwaomba tupendane, tuwe kitu kimoja, tushikamane tusigombane sisi kwa sisi kama tukifanya hivo hakuna jambo litafanikiwa tusiupoteze umoja wetu uchaguzi ulishapita sasa hivi ni wajibu wetu kushikamano, kupendana tukifanya hivo tutaijenga jumuiya yetu”.

Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjni  Bi. Doris Yotham Kibabi amesisitiza juu ya uhai wa jumuiya kwenye matawi na kata kwa ujumla kuhakikisha viongozi wanaongeza au kusajiri wanachama wapya kwa  lengo la kuimarisha ama kudumisha  jumuiya hiyo.

Katibu huyo Bi. Doris Kibabi amewakumbusha viongozi na wanachama wa jumuiya hiyo kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo amewasisitiza pia kutokuwa kwenye sehemu ya kukwamisha maendeleo katika miradi inayotekelezwa na viongozi wa kata, wilaya ya Taifa kwa ujumla.

“Kitu cha kwanza mnatakiwa kwenda kusimamia uhai wa jumuiya kata hii wanachama waliosajiriwa ni wachache mno, mnatuvunja moyo fanyeni vikao vya ndani ninyi makatibu wa matawi mtatue hii changamoto lakini niwaombe tuache makundi kwenye chama chetu tuwe kitu kimoja tushirikiane”.amesema katibu wazazi Wilaya

“Serikali inajengwa na wanachama wa chama cha mapinduzi pamoja na wananchi wetu lakini tujivunie mafanikio ambayo yanaletwa na viongozi wetu wa serikali inayoongozwa na Mama Samia lakini pia juhudi za Mbunge, juhudu za madiwani kwahiyo pale ambapo inatakiwa nguvu ya wananchi tushirikiane, tuwe wa kwanza kuhamasisha maendekleo tusiwe wa kwanza kukwamisha maendeleo tunakosea sisi ndiyo tunatakiwa tuiunge mkono serikali yetu kufanikisha mambo mbalimbali”.amesema katibu Bi. Doris

Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Mhandisi James Jumbe amewaomba wazazi na walezi kusimamia maandili kwa watoto kwa kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ili kuwaepusha na wimbi la mmomonyoko wa maadili pamoja na ukatili katika jamii.

Wazazi tunatakiwa tuwe na uchungu ukisikia jambo la ukatili kuna watu wanataka kulikwamisha lisiende mbele wewe uwe wa kwanza kulipigia kelele kwa ngumu kwa sababu ndiyo jukumu la mzazi”.

“Tukemee mapenzi ya jinsia moja kwenye jamii yetu tuwalinde watoto wetu tusiwalaze na wageni chumbani tuwape elimu watoto na tuwafanye kuwa marafiki ili wakifanyiwa ukatili hata kule shuleni atakwambia mapema bila uoga tupambane kuupinga ushoga pamoja na uzagaji tusiruhusu shetani apite kwenye familia yetu”.

Nao baadhi ya viongozi na wanachama wa jumuiya ya wazazi kata ya Ibadakuli pamoja Kolandoto wameipongeza kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini kwa kufanya ziara hiyo ambapo wameahidi kuzingatia maelekezo yote yaliyozungumzwa na viongozi hao.

 

 

 

 

 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi kupitia chama cha mapinduzi CCM, Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko akizungumza kwenye ziara hiyo kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023.

Viongozi mbalimbali.


Amosi Gombo akikibidhi risala kwa Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Fue Mrindoko  leo Mei 11,2023Jumuiya ya wazazi kata ya Ibadakuli.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi kupitia chama cha mapinduzi CCM, Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko akizungumza kwenye ziara hiyo kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi kupitia chama cha mapinduzi CCM, Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko akisisitiza juu ya usajiri wa wanachama wapya kata ya Kolandato.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi kupitia chama cha mapinduzi CCM, Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko akisisitiza juu ya usajiri wa wanachama wapya kata ya Kolandato.

Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Mhandisi James Jumbe akizungumza na jumuiya ya wazazi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023.

Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Mhandisi James Jumbe akizungumza na jumuiya ya wazazi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023.

Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjni  Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza na jumuiya ya wazazi  kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023 wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji Wilaya.

Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjni  Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza na jumuiya ya wazazi  kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023.

Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjni  Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza na jumuiya ya wazazi  kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023 wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji Wilaya.Share To:

Misalaba

Post A Comment: