Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi  UVCCM wilaya ya Arusha Ndugu Hassan Mndeme ameendelea na ziara yake ya kuhuisha uhai wa Jumuiya kwenye kata zote 25 za Arusha ambapo leo hii ametembelea Kata ya Moshono.

Katika ziara hiyo Mwenyekiti alipokelewa na kufanya kikao Cha Ndani na Kamati ya Siasa kata, kamati ya Utekelezaji kata na Baraza la kata.

Vikao hivi vya ndani pia vilihusisha viongozi Mbalimbali wa serikali wakiongozwa na Mh Diwani wa Kata, Afisa Mtendaji wa Kata, afisa kilimo na watendaji wa mitaa kwa lengo la kuboresha mahusiano baina ya Jumuiya na Serikali na kupata ufafanuzi wa moja kwa moja kwenye mambo yanayohusiana na Fursa za vijana kwenye mitaa na kata.

Aidha Mwenyekiti na ujumbe wake  walipata wasaa wa kutembelea vijana wa Bodaboda katika kata hiyo, kutembelea Mradi wa Green House ambao ni matokeo ya Juhudi za serikali ya awamu ya 6 katika kuwakwamua vijana kupitia fedha zinazotoka mfuko wa OFISI ya waziri Mkuu.

Mwisho Mwenyekiti alipata wasaa wa kuzindua shina la wakereketwa lililopo mtaa WA Moshono kati.

Mwenyekiti ameendelea kusisitiza vijana kuendelea kuchangamkia fursa zinazotokana na Serikali yetu ili waweze kujikwamua kiuchumi. Aidha amewataka viongozi wa Jumuiya kuwa daraja la kuwasaidia vijana kuzitambua fursa hizi na kuzifikia.

Share To:

Post A Comment: