Mhifadhi Robert Faustine  katika shamba la miti Meru USA ambalo lipo chini ya TFS, wakiwa  wameshiriki kwenye zoezi hilo la upandaji miti  kutokana na umuhimu wa pekee haswa katika mifumo ya Ikolojia.

Mkurugenzi mtendaji wa Arusha Dc Suleiman Msumi akizungumza na baadhi ya wanakijiji cha Losikito pamoja na wanafunzi katika shule ya msingi)Sekondari umuhimu wa kutunza. Mazingira

Fransis Nyamhanga ni Afisa Mzingira Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa  Mazingira Kanda  Kaskazini (NEMC):Sisi ni wadau wakubwa sana wa mazingira kwahiyo tunapokuwa na wadau kama hawa wanakuja kusapoti masuala ya uhifadhi wa  mazingira tunafurahi. 

Damian Sulumo ni afisa program wa vikundi vya wakulima na wafugaji( MVIWAARUSHA) Anasema kuwa halmashauri ya Arusha ni wilaya amabayo imeumia na mabadiliko ya tabia nchi hivyo wanalo jukumu la kutunza mazingira

Mkurugenzi mtendaji wa Arusha Dc Suleiman Msumi akipanda mti kama muendelezo wa kampeni hiyo 
Mwanafunzi wa darasa la
 saba  Jeremia samweli aipanda mti kama muenelezo wa kampeni hiyo inayomtaka kila mtu kufanya hivyo na kuhakikisha kuwa anautunza hadi unakuwa mkubwa 


Na.Vero Ignatus,Arusha

Mwendelezo wa Kampeni ya upandaji miti katika halmashauri ya wilaya ya Arusha umezidi kushika kasi ambapo leo tar 11/4/2023  Zaidi ya miti 10,000 ya aina mbalimbali imeoteshwa katika  Kijiji cha  Losikito na Imbibia,ikiwa kampeni hiyo  ni endelevu yenye  kauli mbiu isemayo ''Mti wangu Taifa langu mazingira yangu kazi iendelee''

Akizunmza wakati wa upandaji miti katika shule ya Msingi/ sekondari Losikito Mkurugenzi mtendaji wa Arusha Dc Suleiman Msumi alisema kuwa dhamira kuu ni  kutokomeza tatizo la ukame,kutunza vyanzo vya maji, pamoja na kutunza mazingira ambapo  kila mtu anapaswa kupanda miti na kuwa na zoezi endelevu na kuhakikisha kuwa mti uliopandwa unatunzwa  hadi unakuwa mkubwa

‘’Hapa shuleni kila mwanafunzi anapaswa kupanda mti wake na kuhakukisha kuwa anautunza hadi anamaliza elimu ya msingi,sambamba na wanafunzi wa sekondari nao wanatakiwa kufanya  hivyohivyo kwasababu tunataka tuwe na miti mingi tutunze mazingira yetu tupate mvua zenye tija na kuepuka majanga yasiyokuwa na sababu yeyote’’Alisema Msumi.

Msumi amesema kuwa wamefanya hayo kwa kutekeleza maagizo ya viongozi wa nchi  Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ,ambaye ni mdau mkubwa wa utunzaji wa mazingira kwani tangia akiwa makamu wa Rais aliweza kuendesha kampeni mbalimbali ikiwemo ile ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani, hivyo na wao wameitikia wito wa kutunza mazingira kwa kupanda miti,pamoja na Waziri mwenye dhamana ya Maziringa na Muungano Dkt.Suleiman Jafo alisisitiza kila Halmashauri shule,taasisi,kuanza ngazi ya familia lazima kupanda miti

Katika kupanda miti kupanda miti kuna masuala mawili lakwanza ni kupanda miti lingine je hiyo miti itaendelea kudumu ,itaendelea kukua? Hivyo kila mmoja anao wajibu wa kuhakikisha miti hiyo tunaihudumia hadi inakuwa mikubwa ikitokea imekufa basi tunabadilisha na kupanda mti mwingine mbadala .Alisema Msumi

Akizungumza kwa niaba ya Kamishana ya Uhifadhi Tanzania Profesa Silayo ,Mhifadhi Robert Faustine  katika shamba la miti Meru USA ambalo lipo chini ya TFS, amesema kuwa wameshiriki kwenye zoezi hilo kutokana na umuhimu wa pekee haswa katika mifumo ya Ikolojia ambapo wao wanahudumia shamba la miti Meru ambapo wanatunza mimea bayounuai,vyanzo vya maji pamoja na udongo

Ni wajibu wetu kuhakikisha tunatunza mnyororo mzima wa Ikolojia ili kila mmoja aweze kunufaika na vile vyanzo vya maji mimea pamoja na mazingira safi yanayofanaa kwa afya ya kila mtu,tunashiriki kwa kugawa miti,na kutatoa wito kwa kila mtu mmoja kutunza miti hiyo.

Fransis Nyamhanga ni Afisa Mzingira Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa  Mazingira Kanda  Kaskazini (NEMC):Sisi ni wadau wakubwa sana wa mazingira kwahiyo tunapokuwa na wadau kama hawa wanakuja kusapoti masuala ya uhifadhi wa  mazingira tunafurahi na kuwatia moyo ndiyo maana tumefika maeneo haya kushirikiana na wadau hawa wanaochochea sana ikolojia ilikuhakikisha kwamba tunalima lakini wakati huohuo tunahifadhi mazingira

Aidha ametoa Rai kwa wananchi kuhakikisha kuwa miti waliyoipanda wanaitunza ili ije kuwa faida kwao na kwa kizazi kijacho baadae ,kutakuwa hakuna maana yeyote kama tunapanda miti halafu miti hiyo isitunzwe.Alisisitiza Nyamhanga

Damian Sulumo ni afisa program wa vikundi vya wakulima na wafugaji( MVIWAARUSHA) Anasema kuwa halmashauri ya Arusha ni wilaya amabayo imeumia na mabadiliko ya tabia nchi hivyo wanalo jukumu la kutunza mazingira kwa kupanda miti hadi itakapofikia mwisho wa mradi wao KILIMO ENDELEVU wawe wameweza kufikia hekta 60 sawa na heka 160,hivyo wataendelea kuhamasisha wakulima na wafugaji waweze kupanda miti maeneo ya wazi na mashambani na kutunza mazingira

Aidha amesema kuwa mradi huo unawezesha shughuli hizo sambamba na wadau wengine waliopo kuweza kuhakikisha wanafanya shughuli nyingine za uzalishaji ambapo shughuli hiyo ni ya mwendelezo

 Ayesiga Buberwa ni meneja miradi wa shirika la ISLAND OF PEACE,pamoja namashirika mengine mawili  wanatekeleza mradi wa kilimo endelevu Arusha unaolenga kukuza na kuendeleza kulimo ekolojia kwa watu pia linaangalia chakula kinapoanza shambani hadi kinapofika  kwa mlaji mazingira yanayomzunguka sambamba na utunzaji na uhifadhi wa mazingira

Buberwa amesema kuwa wanaangalia mifumo yote ya uzalishaji wa chakula pamoja na ile ya kuhifadhi mazingira kwamba mradi huo unaangalia kuuhisha katika hali ya kawaida mazingira ambayo yameharibika il mkulima aweze kulima vizuri pamoja na mfugaji aweze kufuga vyema pia na malaji aweze kupata chalila safi na salama.

Share To:

Post A Comment: