“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kibali cha kuajiri watumishi 21,200 wa Kada za Ualimu  na Afya. Idadi ya Watumishi watakaoajiriwa katika Kada za Ualimu ni 13,130 ambao watafundisha katika shule za Msingi na Sekondari. Aidha idadi ya watumishi watakaoajiriwa katika kada za Afya ni 8,070 ambao watafanya kazi katika Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati”.


Angellah Kairuki

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI

12.04.2023

Share To:

Post A Comment: