Ikiwa imepita saa chache tangu kufutiwa kesi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jatu PLC, Peter Gasaya (33) amefikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kusomewa kesi ya Uhujumu uchumi yenye mashtaka mawili ambayo ni kujipatia fedha kiasi cha Sh 5.1bilioni na kutakatisha fedha.

 Gasaya amesomewa mashtaka hayo leo Alasiri, April 11, 2023 na wakili wa Serikali, Adolf Verandumi mbele ye Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo.

Itakumbukwa kuwa leo, mapema majira ya saa sita mchana, mshtakiwa huyo alifutiwa kesi ya jinai namba 207/2022 na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) baada ya kueleza Mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendea na shauri hilo.

Hata hivyo muda mfupi baadae mshtakiwa huyo alikamatwa na kuwekwa chini ya uangalizi wa Askari Polisi waliopo katika Mahakama hiyo.

Share To:

Post A Comment: