Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo mwenye kanzu nyeupe akiwa sambamba na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya hiyo wakimfariji mama aliyeondokewa na mpendwa mme wake.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo mwenye kanzu nyeupe akiwa sambamba na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya hiyo wakimfariji mama aliyeondokewa na mpendwa mme wake

Na Fredy Mgunda,Nachingwea


MTU mmoja anaejulikana kwa jina la Mstaafa Mkane mwenyewe umri wa miaka 60 ameuwawa na mnyama Tembo katika Kijiji cha Ngunichile kutokana na kundi kubwa la wanyama hao kuvamia mashamba ya wananchi wa Kijiji hicho na vijiji vingine vya kata ya Ngunichile.

Akidhibisha kutokea kwa kifo hicho mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amekiri kutokea kwa kifo cha mwananchi wa Kijiji cha Ngunichile kutokana na kuvamiwa na mnyama Tembo.

Moyo alisema kuwa tarehe kumi usiku alipokea simu kutoka kwa afisa Tarafa ya Lionjo kuwa kuna mwananchi amekufa kutokana na kuvamiwa na mnyama Tembo hivyo serikali walianza kuchukua hatua ya kuhakikisha wanauzika mwili huo na baada ya ndio wakaenda kukutana na wananchi wa Kijiji cha Ngunichile.

Alisema kuwa serikali imechukua hatua ya kuongeza idadi ya askari wa TAWA ili kuwafukuza Tembo hao ili wasilete madhara mengine kwa wananchi kama walivyosababisha kifo cha mwananchi huyo.

Moyo alisema kuwa kutokana na kifo hicho na kuharibiwa kwa mashamba ya wananchi wa Kijiji cha Ngunichile serikali ya wilaya ya Nachingwea imetoa tani 20 za chakula kwa ajili ya wananchi ambao wameadhika kutokana mnyama Tembo kuvamia mashamba ya wananchi hao.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Ngunichile Said Makayola ameiomba serikali kutafuta njia ya kudumu kuwaondoa Tembo hao katika kata hiyo kutoka na kuleta madhara makubwa kwa wananchi wanaoishi katika kata hiyo.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: